Dar Es Salaam,Tanzania.
Habari za uhakika ambazo tumezipata kutoka katika chanzo cha uhakika ndani ya Yanga zinaonyesha kuwa mwenyekiti wa Yanga,Yusuf manji,ameamua kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti pamoja na kusitisha kusudio lake la kuichukua na kuendesha kibiashara timu ya Yanga na nembo yake .
Hili ni anguko kuu kwa yanga endapo Yusuf manji atajionda Yanga kutokana na ukweli kuwa tayari mahasimu wao wa jadi Simba wanakamilisha taratibu za kumkabidhi timu,Mohamed Dewji MO.
Uamuzi wa Manji kujiondoa Yanga unatajwa kuchangiwa na shutuma zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa serikali na wengine kutoka ndani ya Yanga ambao wanatumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kwa maslahi yao binafsi na sio ya Yanga.
Manji anaonekana kuchoshwa na tabia za baadhi ya watu kumtukana na kumkebehi kwa hatua yake ya kuichukua timu ya Yanga na sasa ameamua kukaa pembeni kulinda heshima yake.
Hata hivyo viongozi wa Secretary ya Yanga siku nzima ya leo wameonekana
kuchanganyikiwa huku baadhi wakiwa wanapigana vikumbo kuingia na kutoka
Quality Plaza zilizopo ofisi za Manji hatua inayoashiri kuna jambo kubwa linatokea.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment