Mwanamke Siddiqa Parveen mwenye umri wa miaka 28 ambaye ni raia wa India, kwa sasa ndiye anashikilia rekodi ya kuwa mwanamke mrefu kushinda wote Duniani akiwa na urefu wa futi 7.8(238Cm).
Awali, Siddiqa alikuwa akisumbuliwa na uvumbi uliokuwepo katika ubongo wake ambao ulikuwa unamfanya aendelee kurefuka siku hadi siku hivyo kumlazimu kutembea umbali wa maili 1000 kutoka kijiji alichokuwa anaishi kilichopo Bengal magharibi hadi mji mkuu wa nchi hiyo New Delhi kutafuta mwarobaini wa tatizo lake.
Daktari Ashish Suri ambaye alikuwa miongoni wa jopo la madaktari waliohusika na zoezi la kumfanyia operesheni Siddiqa, anaeleza changamoto walizokumbana nazo wakati wanamfanyia zoezi la kuondoa uvumbe kwenye ubongo wake ikiwemo umbo lake kuwa kubwa hivyo kuleta shida wakati wa zoezi hilo na piakuwalazimu kuongeza ukubwa wa kitanda.
Mwanamke huyo ameingizwa kwenye Guinness Book of Records kwa mwaka wa 2014 kwa kushikilia rekodi ya kuwa mrefu kwa upande wa wanawake. Ivyo kama Mwanadada Siddiqa Parveen angeamua kushiriki ligi kuu ya mpira wa kikapu Marekani(NBA) ndiye angekuwa mchezaji mrefu kuliko wote huku akimuacha Mtanzania Hasheem Thabeet(7Ft 3/221cm) ambaye ndiye mchezaji mrefu kuliko wote katika ligi hiyo kwa sentimita 16.
Siddiqa akiwa na baba yake.
Hapa akiwa na wazazi wake wote wawili.
Pichani ni Siddiqa akiwa hospitalini kipindi alichofanyiwa operesheni hivyo kuwalazimu kuongeza urefu wa kitanda.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment