Waswahili wanasema ukistaajabu ya mussa utayaona ya firauni na kushi kwingi ni kuona mengi, hatimaye wanandoa wanne ambao ni mapacha wawili wa kike na mapacha wawili wa kiume wameweza kuingizwa katika kitabu cha kuhifadhi kumbukumbu kubwa za Dunia kinachofahamika kwa jina la Guiness Book Of World Records baada ya kufunga ndoa siku moja Tarehe 30 mwezi Novemba 2013 nchini Nigeria.
Kwa mujibu wa Guinness Book of World Records imetangaza kwamba Ndoa hiyo iliyohusisha Mapacha wa kike wawili wanaofanana(Identical Twins) kufunga ndoa na mapacha wenzao wa kiume(Identical Twins) imekuwa ya kwanza kufungwa katika bara la Afrika huku ikikamata nafasi ya Ishirini na tano(25) kwa Dunia, Wanandoa hao ambao ni Omole na Ikeja ambao ni mapacha wanaofanana wakiume sambamba na wake zao Folawemi Taiwo Okunniyi na Febisola Kehinde Okunniyi waliungana pamoja na kisha kufunga ndoa yao katika kanisa la kiinjili la Foursquare kisha tafrija kufanyika katika ukumbi wa 10 Degree Events Centre uliopo eneo la Oregun Nigeria.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment