MWANDISHI WETU,
DAR ES SALAAM: Hii ni ajabu na kweli! Vijana wawili waliofahamika kwa jina mojamoja la Mudi na Thomas, wakazi wa Mtaa wa Udzungwa, Sinza jijini Dar, wamenusurika kifo baada ya kudaiwa kushindana kunywa mizinga mikubwa miwilimiwili ya konya na midogo miwilimiwili (jumla nane) kisha viroba nane vya pombe kali (ngumu kumeza) hivyo kuzimika na kujisaidia hadharani kwenye nguo.
Mashuhuda walilieleza Wikienda kwamba, tukio hilo la kusikitisha na la aibu lililozua sintofahamu kwa wakazi wa Sinza, lilijiri juzikati baada ya vijana hao kutandika vinywaji hivyo ambavyo vilitolewa ofa.
“Washkaji walikuwa wanapiga mtungi mdogomdogo. Mara akaibuka mshkaji mmoja na kuwapa ofa ya mizinga mikubwa miwilimiwili na midogo yake kwa kila mtu kisha akawaongezea viroba vinne kwa kila mtu.
“Baada ya kupewa ofa, jamaa waliendelea ‘kugambeka’ ili kumpata bingwa atakayechukua dau la Sh. 45,000 lililowekwa mezani na ‘promota’ huyo aliyedhamini mpambano huo haramu.
“Baada ya kufuta mzigo, hali zao zilikuwa mbaya kiasi cha kushindwa kutembea na kuishia kudondoka kabla ya kuzimika jumla.
“Walizimika saa 9:00 alasiri hadi alfajiri ya siku iliyofuata, jambo lililosababisha watu kuhisi wamekata roho kwani mmoja wao alikuwa anahema kwa mbali.
“Pamoja na mmoja wao kuibuka mshindi (haikufahamika kama ni Mudi au Thomas) lakini hakuweza kuchukua Sh. 45,000 yake kama mshindi kwa sababu alizimika kabla hajakabidhiwa fedha zake,’’ alisema mmoja wa mashuhuda hao.
Hata hivyo, wakazi wa mtaa huo walimshangaa mmoja wa vijana hao ambaye ilisemekana ni baba wa familia lakini anaendekeza mambo ya ulevi.
“Hii ni ajabu na kweli. Ni tukio la kujidhalilisha na lisilokubalika kwenye jamii, mtu una familia halafu wanaitwa wakuone ulivyolewa na kujisaidia hadharani ni aibu sana,” alisema mama wa makamu aliyeshuhudia tukio hilo na kuongeza:
“Pombe zinaua vijana kwa sababu za kijinga kabisa, mimi nakemea kwa nguvu zote unywaji wa pombe uliopitiliza kwenye jamii.”
Kwa upande wao vijana hao walipofuatwa mtaani hapo kesho baada ya ‘kufufuka’ waligoma kuzungumza chochote kwa aibu, kila mmoja akidai ni mzima wa afya.
Tukio kama hilo liliwahi kutokea siku za nyuma maeneo hayohayo ambapo kijana mmoja alitamba kuwa ni mkali wa kunywa ngumu kumeza lakini kama siyo kukimbizwa Hospitali ya Sinza-Palestina, angekata roho kama ilivyotokea kwa wengine waliowahi kuzidisha kinywaji hicho hivyo unywaji wa pombe za sampuli hiyo ni kujitafutia kifo
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
About Rafiki Fm Ludewa
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment