CHUPI YA SHANGAZI SEHEMU YA 2


 Nilirudi kuketi pale kitandani kwangu kama zuzu aliyepoteza kumbukumbu huku nikitafakari lile jambo nililoliona pale nje kupitia dirisha langu........nilitafakari kwa muda mrefu kidogo,mpaka nilipo shutshwa na sauti kali kutoka nje,mihogooo.....kibanda meno....haya mihooogo,alikuwa ni kijana anayefanya biashara ya mihogo mibichi na mara kwa mara hupita pale nje ya nyumba yetu asubuhi  subuhi,kuwaauzia watu wa kijiji chetu vitafunwa vya chai,hasa ukizingatia watu wengi wa kijiji chetu,hawana uwezo wa kupika au kununua chapati,na waliokuwa na uwezo wengi hupendelea mihogo kutokana na shughuli zao ngumu za shambani,hivyo kijana yule alikuwa na uhakika na soko la bidhaa yake hiyo pale kijijini kwetu.
  Niliamka taratibu nikachukua mswaki wangu uliokuwa umechakaa chakaa na kunyambuka nyambuka nyuzi zake kama nywele za mkichaa kutoka milembe,pembeni nilitazama kiti changu kibovu nilichokuwa nakitumia kama meza yangu,niliyokuwa naitumia kuwekea makorokoro yangu kama viwembe,saa mbovu na manati yangu,nilitazama buibui zilizojaa pale chumbani kwangu,kabla ya kutoka nje ya nyumba na kuchukua kopo la kunawia uso,lililokuwa katika pipa kuukuu pale nje ya nyumba yetu,kisha nikachota maji katika mtungi uliokingwa sawa na bati la nyumba yetu ili kupata maji ya mvua,kipindi cha msimu wa mvua,wakati naendelea kusafisha kinywa changu nilisikia njorogee......njorogee...niligeuka nyuma kutizama kule sauti inapotoka....nilimuona kijana mrefu mweupe..aliyevaa kofia ya baragashia akija kwa madoido kule nilipokuwa nasafisha kinywa changu,nilimtazama vizuri alikuwa ni juma mpemba,rafiki yangu niliyesoma nae darasa moja na tulihitimu wote kidato cha nne...alisogea mpaka pale nilipokuwa kisha akanisabahi...sheikh assalam aleikum,niliitikia huku nikimsogelea waalekum musalam maalim,...haya mambo vipi kaka aliniuliza bwana juma mpemba,ambae shuleni alikuwa akitumia jina la juma mohammedi hilo la mpemba alipewa na watu kutokana na yeye asili yake ni mtu kutoka huko visiwani pemba....nilimjibu kaka huku ni kwema sijui huko,alinijibu huku akitabasamu lakini aliyeonekana mwenye kusita kidogo....nikamwambia kaka ni muda mrefu sana hatujaonana haya nipe kaifa,akaniambia kaka nimekuja na suala langu unipatie mawazo,nikanyanyuka kidogo na kwenda kuuweka mswaki wangu pale katika kiti changu kibovu mle chumbani mwangu,kisha nikarudi nje na kuvuta benchi dogo lenye vumbi na kulifuta futa,nikamwambia juma mpemba sheikh karibu...aliketi na kuvuta pumzi kidogo....akasema bwana njorogeee...mambo magumu kaka..nilimtazama usoni kwa umakini kijana yule aliyekuwa na muonekano mzuri,licha ya kuwa na meno yaliyooteana na kupandana upande wa kulia mbele ya kinywa chake,lakini hilo halikuharibu muonekano wake,mpaka pale alipofungua kinywa kucheka,mambo hayaendi kabisaaa...sipati wateja kaka yaani hapa nina shilingi elfu tu...nimeambiwa mpaka nioe kaka....kwa kila mtaalamu niliyekwenda ameniambia hivyo......alimalizia juma,juma alipomaliza kidato cha nne,na hakuweza kuendelea na masomo licha ya kuwa na cheti kilicho ridhisha kidogo....baba yake mzee mohammedi yeye alikuwa ni mganga wa jadi anayetumia vitabu vya kuran,kwa muda mrefu kusaidia baadhi ya watu wenye matatizo na walioamini kusaidiwa na njia hiyo ya imani,baadae alifariki na aliwaacha juma na ndugu zake  watatu wa tumbo moja licha ya kuwa mzee huyo alizaa watoto wengi ambao ni watu wazima nao aliwaacha huko visiwani pemba kabla ya kuja huku kijijini kwetu,mzee huyo hakufanikiwa kujenga hata kibanda licha ya kuwa alipata visenti vingi enzi za ujana wake,alishindwa kuwaendeleza akina juma kimasomo kutokana na umri kuwa umemtupa mkono kwani,aliwazaa akina juma akiwa tayari mtu mzima,wakati juma anamaliza kidato cha nne mzee huyo alianza kupata maradhi na kuugua,hali iliyompelekea juma,kufanya kila aina ya kazi kukidhi mahitaji yake,alichimba mashimo ya choo,aliuza maduka ya watu na kufanya kila aina ya kazi,lakini kutokana na juma kupata kidogo elimu ya kiarabu aliposoma madrasa,alijua kusoma na kuandika lugha hiyo ,hivyo baba yake alipokuwa mgonjwa alikuwa akimpa maelekezo juma na kuwashughulikia wateja waliokuwa wanakuja hapo kilingeni kwake,hivyo juma aliweza kupata ujuzi kidogo...hata kipindi baba yake alipozidiwa na kupelekwa kwao pemba kwa ajili ya matibabu,juma alibaki pale kwenye nyumba ile wanayoishi,ilikuwa ni nyumba ya kupanga mzee juma aliyoishi na familia yake kwa zaidi ya miaka 25,na baadhi ya watu walidhani ni nyumba yake lakini haikuwa kweli....hapo ndipo palipokuwa kilinge cha mzee mohammedi,wageni walipofika pale walimkuta juma ambaye aliwaambia baba yake hayupo na yeye angeweza kuwasaidia, mzee mohammedi alimwamini sana juma hasa katika uhodari wake wa kusoma na kuandika lugha ya 
kiarabu...mzee mohammedi alipofariki juma mpemba kwa ugumu wa maisha alidhani uganga ingekuwa kazi rahisi kwake ya kumwendeshea maisha.
        nilimuuliza juma je umejiaanda kwa ajili ya kuoa?...umejipanga?na maisha haswa ukizingatia maisha ya sasa ni magumu sana juma alinijibu kwa hamaki....ndio maana nimekuja kwako kaka unipatie mawazo maana mambo hayaendi kabisa...



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: