Kikosi cha Simba kilichoanza mtanange wa leo dhidi ya AFC Leopards.
Kikosi cha AFC Leopards kilichoanza dhidi ya Simba leo.
Ibrahim Ajib wa Simba akijaribu kumtoka beki wa AFC Leopards, Edwin Wafula.
Wachezaji wa Simba wakishangilia mojawapo ya mabao yao.
Laudit Mavugo wa Simba akizuiwa na ngome ya AFC Leopards.
Mashabiki wa Simba wakishangilia ushindi wao.
Mavugo akishangilia bao aliloifungia Simba.
Mwenyekiti wa Simba, Evans Aveva akilishwa keki.
Mgeni rasmi wa hafla ya leo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akilishwa keki katika sherehe za Simba Day.
Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ naye akilishwa keki.
Mlezi wa Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ akilishwa keki katika sherehe hizo.
Klabu ya Simba leo imesherehekea vizuri miaka 80 tangu kuanzishwa kwake kwa kuishushia kichapo cha mabao 4-0 timu ya AFC Leopard kutoka nchini Kenya.
Sherehe hizo maarufu kama Simba Day, zimefanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Simba iliwatambulisha wachezaji wake wapya ambao imewasajili kwa ajili ya msimu wa 2016/17.
Mbali na utambulisho huo, Simba walikata keki na kuwalisha baadhi ya viongozi wa timu hiyo na waasisi wake sambamba na mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mabao ya Wekundu wa Msimbazi yamewekwa kimiani na Ibrahim Ajib aliyetupia mawili huku bao la tatu likifungwa na Shiza Kichuya na bao la mwisho kufungwa na mchezaji mahiri Laudit Mavugo
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
About Rafiki Fm Ludewa
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment