kabila lako Asili ya falme za makabila ya Afrika-II


KATIKA toleo lililopita tupata historia ya kabila la Waha linalopatikana mkoani Kigoma. Leo tunaendelea na simulizi za makabila mengine kadiri inavyosimuliwa na ukurasa wa Historia ya Afrika.
KABILA WADOE
Wadoe ni moja ya kabila linalopatikana maeneo ya Pwani hasa maeneo ya Pumbuji (Bagamoyo ya sasa) na maeneo mengine ya Pwani hasa mkoani Tanga, maeneo ya Handeni. Wadoe wanapatikanba kwenye familia lugha ya kibantu na lugha yao ni kidoe.
Wadoe walitokea katika kundi la Wabantu wa mashariki waliofika maeneo haya kabla hata ya miaka ya 1400. Walipata kuishi maeneo hayo kwa muda mrefu sana.
Kabila hili lilikuwa kubwa sana kwa wakati huo, lakini kama ilivyokuwa kwa Wazigua, kabila hili liligawanyika sana . Mgawanyiko wao ulisababishwa na vurugu na vita vilivyokuwa vikianzishwa na Wazigua kwa wakati huo.
Historia inafafanua hivi, licha ya vita vilivyokuwa vikianzishwa na Wazigua, bado biashara ya utumwa ilisababisha kupungua kwa idadi ya watu. Kwani Wazigua walikuwa wakiwakamata Wadoe na kuwauza kwa Waarabu waliokuwa wakiishi katika maeneo ya Ukilindi.
Na ifahamike kuwa kwenye miaka ya 1800, Wadoe walionekana kuwa na tamaduni ambazo hazifanani na makabila mengine yaliokuwa yakipatika pembezoni mwa kabila hilo.
Na kikubwa cha kufahamua juu ya kabila la wadoe ni kwamba, Kwenye miaka ya 1886 kulitokea mzungi mmoja aliyefahamika kwa jina la Brunner alisema kuwa, Wadoe walipata kuhama kutoka maeneo ya Pwani na kufika maeneo ya Mombasa.
Lengo la kufika huko lilikuwa ni kukimbia vita na biashara ya utumwa iliyokuwa imeshamili kwa wakati huo. Ukweli ni kwamba wadoe hao hawakupata kufahamika zaidi kwenye maeneo hayo kwani walifika wakiwa wachache sana.
Sababu ya kufika wachache ni kwamba, wakati Wadoe wanaenda Kenya, humu njiani kulikuwa na makabila kama Wamasai waliokuwa na mori ya kupiga vita na makabila kama Wapare.
Hivyo kuna
sehemu
Wadoe walijikuta wakiingia kwenye vita hivyo na kujichanganya na makabila hayo. Na sababu nyingine ni kwamba, makabila mengi ya Afrika yalipata majina kulingana mitazamo ya wageni na wenyeji waliowakuta kule.
Hivyo Wadoe waliopata kufika Kenya walitambuliwa kwa jina linguine na sio la Wadoe. Kwani asili ya neno wadoe ni huku huku Tanzania. Na pia hata kwa wakati huo kulikuwa na kabila kama Wagiriama, ambao waliweza kukuwa kutokana na ujio wa Wadoe kwa wakati huo na ushahidi wa kufanana kwa tamaduni kati ya Wagiriama na Wadoe hasa katika suala la ndoa za kimila.
Hivyo Wadoe hawakujilikana kwenye ardhi ya Kenya kutokana na kuchanganyana na makabila waliyoyakuta. Yaani historia hii inafanana na ile ya Wagogo, kwani Wagogo ni mchanganyiko wa makabila mengi. Kwa ujumla kabila hili historia yake haikuandikwa sana na kabila hili limeelezewa kutoka kwenye makabila mengine. Na kama kuna maandiko kuhusu Wadoe wakati ndio huu. Historia yetu hipo na sisi ndio wa kuijenga.
KABILA LA WARORI NA WAHEHE
Kabila la Warori ni moja ya kabila ambalo lilipata kukua na kuwa na nguvu kuzidi hata Wahehe kwenye miaka ya 1700. Habari za kabila la Warori lilipatwa kusimuliwa na kuandikwa na Waingereza kama John Speke na Richard Burton mnamo miaka ya 1840. Na baaadae kuja kufanyiwa tafiti na East African Bureau miaka ya 1930.
Ukweli ni kwamba kabila hili lilipata kuishi maeneo ya upande wa magharibi mwa ardhi ya Uhehe. Na pia Warori walifanikiwa kufika mpaka maeneo ya mto Ruaha na mpaka kufika maeneo ya Unyanyembe. Wakati kabila hili linakuwa lilikuwa linapenda sana vita.
Na inasemekana hata Wahehe walikuwa wanawaogopa Warori, kwani Warori walikuwa wametapakaa kwenye maeneo yote na walikuwa na wanajeshi wa kutosha. Na inasimuliwa kuwa Wahehe kwa wakati huo hawakuwa na nguvu kama inavyofahamika kwani wakati huo walikuwa bado hawajasambaa sana. Na pia wakati ambao Wangoni walikuwa bado hawajafika.
Warori walikuwa wakifanya biashara na makabila kama Wafipa. Wakati huo Wafipa walikuwa wataalamu wa kufua vyuma.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: