IGAD;Sudani Kusini yaridhia kutumwa kikosi cha kanda



mediaRaisi wa Sudani kusini Salva KiirREUTERS/Stringer
Sudani Kusini imekubali kutumwa kwa jeshi la kikanda baada ya kuzuka kwa mapigano mapya kati ya vikosi vya raisi Salva Kiir na aliyekuwa kiongozi wa waasi Rieck Machar viongozi wa IGAD wamethibitisha.
‘’Serikali ya Sudani kusini imekubali’’alisema Mahboub Maalim na kuongeza kuwa idadi kamili ya kikosi hicho bado haijapangwa.
Aidha makubaliano yakishafikiwa kuhusu uamuzi huo yatafikishwa katika baraza la usalama la umoja wa mataifa ili kupigiwa kura.
Viongozi wa kikanda kutoka baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki walikutana jana jijini Addis Ababa, nchini Ethiopia kujadili mzozo wa Sudan Kusini, na namna ya kuingilia kati kuusuluhisha mzozo huo kwa njia ya kijeshi.
Marais hao kutoka mataifa wanachama wa IGAD wamekuwa wakijadili undani wa pendekezo lililotolewa na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika AU la kutaka kutuma vikosi vya usalama nchini Sudan kusini baada ya kuzuka kwa mapigano ya hivi karibuni kati ya jeshi la serikali na vikosi vya aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar




Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: