DRC: Koffi Olomide asalia jela


mediaMwanamuziki maarufu wa DRC, Koffi Olomide mbele ya mahakama mjini Kinshasa tarehe 16 Agosti 2012. (Picha ya zamani)JUNIOR KHANNA / AFP
Koffi Olomide hatimaye amewekwa kizuizini. Wanasheria wake hawakuweza kupata dhamana kwa nyota huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambaye ameshitakiwa kumpiga mmoja wa wachezaji wake nchini Kenya.
Tukio hili lilirekodiwa na limesambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii. Msanii huyu maarufu wa Congo atasalia jela kwa siku zaidi ya kumi na tano. Uamuzi ambo umepingwa na mwanasheria wake Ruffin Lukoo.
Koffi Olomide, alikamatwa jijini Kinshasa kwa kosa la kumpiga teke mnenguaji wake wa kike jijini Nairobi nchini Kenya mwishoni mwa juma lililopita.
Masaibu ya Olomide yameendelea kushuhudiwa kwa juma la pili baada ya kukamatwa na kufukuzwa nchini Kenya kutokana na tukio hilo, na tamasha lake kusitishwa.
Polisi nchini DRC wanasema mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 60 anashikiliwa kwa mahojiano zaidi kutokana na tukio la Nairobi.
Jumapili iliyopita, Olomide alihojiwa na Televisheni moja nchini humo akiomba msamaha kwa kitendo alichofanya.
"Hii sio mara ya kwanza kwa mwanamuziki huyu kujipata katika hali hii", wamesema baadhi yawanenguaji wake waliotengana naye baada ya visa kama hivyo, na kuamua kujiunga bendi nyingine nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: