Barack Obama amkejeli hadharani Donald Trump
Rais wa Marekani katika mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya Pentagon katika mji wa Arlington, Virginia, Agosti 4, 2016.REUTERS/Jonathan Ernst
Donald Trump anasema atashangaa iwapo hatoshinda uchaguzi wa urais nchini Marekani uliopangwa kufanyika mwezi Novemba. Bw Trump anasema ikiwa atashindwa itakua ni kutokana na wizi wa kura uliyopangwa na mpinzani wake.
Kwa mujibu wa Donald Trump, maandalizi kwa ajiliya wizi huo tayari yameanza. Madai ambayo hayajachukuliwa umakini, ikiwa ni katika upande wa chama cha Republican wala Barack Obama, ambaye amemkejeli mgombea huyo.
"Uchaguzi huu utakuwa umekubwa na udanganyifu, watatuibia ushindi wetu," amesema Donald Trump katika mikutano yake ya mwisho. Madai ambayo hayachukuliwi kwa umakini, ikiwa katika upande wa chama cha Republican, au katika cham cha Democratic, lakini madai haya yanawatia wasiwasi wafuasi wa mgombea huyo kwa tiketi ya cham acha Republican. Barack Obama, akihihojiwa juu ya suala hili Alhamisi, Agosti 4, 2016 katika mkutano na waandishi wa habari, alijibu kwa ucheshi.
"Bila shaka, hakutakuwa na udanganyifu. Huu ni ujinga, hakuna mtu atakayechukulia madai haya kwa umakini! Nadhani kila mmoja wetu katika maisha yake, akishiriki mashindano, katika sehemu mbalimbali, tuliwaona watu kama hawa wakipoteza au wakishindwa wanaanza kupiga kelele wakidai kuibia ushindi. Lakini jambo hili ni mara ya kwanza, kuona mtu akilalamika kabla ya mwisho wa mchezo! Ushauri wangu ni: kuacha kulalamika, fanya kinachohitajika iliushinde uchaguzi, " rais Obama amesema.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment