UEFA CHAMPIONZ LIGI: CITY YATAMBA KIEV, ATLETI SARE NA PSV UHOLANZI!


UEFA CHAMPIONZ LIGI
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
JUMATANO 24 FEB 2016
Dynamo Kiev 1 Man City 3
PSV Eindhoven 0 Atletico Madrid 0
+++++++++++++++++++++
CITY-USHINDI-KIEVMANCHESTER CITY imejiweka vyema kutinga Robo Fainali baada ya kupata ushindi mnono Ugenini katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, walipoichapa Dynamo Kiev Bao 3-1 huko Kiev, Nchini Ukraine.
City, ambao walibadili Wachezaji 10 toka kile Kikosi kilichodundwa 5-1 na Chelsea kwenye FA CUP Jumapili iliyopita, walitawala Kipindi cha Kwanza na kupiga Bao 2 kupitia Sergio Aguero na David Silva zilizofungwa Dakika za 15 na 40.
Vitaliy Buyalsky aliipa Bao Dynamo katika Dakika ya 58 na Gemu kuwa 2-1 lakini Yaya Toure akawakata maini katika Dakika ya 90 kwa Shuti murua la kupinda na kufunga Bao la 3 na kuwapa City ushindi mnono wa 3-1 kuelekea Mechi yao ya Marudiano hapo Machi 15 Uwanjani Etihad.
Katika Mechi nyingine ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UCL PSV Eindhoven na Atletico Madrid zilitoka Sare 0-0 huko Mjini Eindhoven Nchini Uholanzi.
PSV walibaki Mtu 10 kuanzia Dakika ya 58 baada ya Pereiro kupewa Kadi Nyekundu kufuatia Kadi za Njano 2.
VIKOSI:
Dynamo: Shovkovskiy, Danilo Silva, Dragovic, Vida, Khacheridi, Rybalka, Garmash, Gonzalez, Buyalskiy, Yarmolenko, Teodorczyk
Akiba: Rudko, Veloso, Petrovic, Moraes, Korzun, Gusev, Makarenko
City: Hart, Sagna, Kompany, Otamendi, Clichy, Fernando, Fernandinho, Toure, Silva, Sterling, Aguero
Akiba: Caballero, Demichelis, Zabaleta, Mangala, Kolarov, M.GarciaIheanacho
REFA: A Mateu Lahoz (Spain)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Marudiano
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza
JUMANNE 8 MAR 2016
Real Madrid v AS Roma [2-0]
VfL Wolfsburg v KAA Gent [3-2]
JUMATANO 9 MAR 2016
2000 Zenit St Petersburg v Benfica [0-1]
Chelsea v Paris St Germaine [1-2]
JUMANNE 15 MAR 2016
Atletico Madrid v PSV Eindhoven [0-0]
Man City v Dynamo Kiev [3-1]    
JUMATANO 16 MAR 2016
Barcelona v Arsenal [2-0]
Bayern Munich v Juventus [2-2]
++++++++++++++++++++++++++++
TAREHE MUHIMU:
Raundi za Mtoano:
-Droo ya Robo Fainali: Machi 18
**Mechi Aprili 5/6 na Marudiano Aprili 12/13
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: