09:56 Magazeti ya Uganda yameongoza na habari za uchaguzi.
07:45 Upigaji kura katika maeneo mengi umeanza, ingawa kwa kuchelewa. Hapa ni Kalangala watu wakipiga kura.
07:44 Kuna ripoti kwamba baadhi ya watu wanaotumia simu kuingia mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook wanatatizika. Lakini WhatsApp inafanya kazi.
07:30 Upigaji kura ulifaa kuanza saa moja asubuhi lakini katika vituo vingi, licha ya wapiga kura kujitokeza, shughuli yenyewe haijaanza na wapiga kura wanalalamika. Katika kituo cha Kamwokya Central Market, vifaa vya kupigia kura vinaingizwa kituoni pole pole. Mwangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Madola Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo amekuwa katika kituo hicho.
Bw Obasanjo anaongoza waangalizi wa Jumuiya ya Madola
07:09 Tuangalie takwimu muhimu kuhusu uchaguzi wa Uganda unaofanyika leo.
Takwimu muhimuWagombea urais8Maeneo bunge290Vituo vya kupigia kura28,010Wapiga kura waliosajiliwa15,277,196
07:00 Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa.
06:40 Wapiga kura wameanza kufika katika vituo vya kupigia kura. Hapa ni katika kituo cha Kalangala, katika kisiwa kilichoko katika Ziwa Victoria.
Wapiga kura 15 milioni nchini Uganda leo wanafika vituoni kupigia kura viongozi wao, kinyang'anyiro cha urais kikivutia wagombea wanane.
Electoral Commission of Uganda
Vituo vya kura vitafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi alasiri
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment