Liverpool itamenyana na mahasimu wao wakubwa, Manchester United katika hatua ya 16 Bora ya Europa League PICHA ZAIDI GONGA HAPA
TIMU ya Liverpool imepangwa kucheza na mahasimu wao, Manchester United katika hatua ya 16 Bora ya michuano ya Europa League.
Huku timu zote mbili zikiwa nje ya nne bora katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, ushindi kwenye mashindano hayo utawapa nafasi ya kufuzu kwenye Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Timu zitamenyana nyumbani na ugenini ndani ya wiki moja, mechi ya kwanza ikipangwa kuchezwa Uwanja wa Anfield Machi 10 na marudiano Old Trafford Machi 17.
Timu nyingine ya England, Tottenham imepangwa kucheza na wababe wa Ligi Kuu ya Ujerumani, maarufu kama Bundesliga, Borussia Dortmund wakati timu ya kocha Muingereza, Gary Neville, Valencia itamenyana na Athletic Bilbao zote za Hispania.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya michuano ya Ulaya Liverpool na Man United kukutana. Liverpool na United ndizo timu za England zenye mafanikio zaidi katika michuano ya Ulaya.

REKODI YA LIVERPOOL DHIDI YA MA UNITED
Zimekutana mara: 177
Liverpool imeshinda: mechi 60 ( sawa na asilimia 33.9)
United imeshinda: mechi 72 ( sawa na asilimia 40.7)
Zimetoka sare mara: 45 (sawa na asilimia 25.4)
Mabao yaliyofungwa 244-228
United imetinga 16 Bora ya Europa League baada ya kuitoa Midtjylland kwa kuifunga jumla ya 6-3
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya michuano ya Ulaya Liverpool na Man United kukutana. Liverpool na United ndizo timu za England zenye mafanikio zaidi katika michuano ya Ulaya.
Liverpool imetwaa Europa League (zamani Kombe la UEFA) mara tatu na Ligi ya Mabingwa mara tano, wakati Man United imetwaa mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na sasa inawania kushinda taji la kwanza la Europa League katika historia yao.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment