MVUA ZAENDELEA KUHARIBU MIUNDOMBINU LUDEWA NA KUBOMOA MADARAJA



 Eneo la daraja maeneo ya mwisho wa lami shule ya sekondari Chief Kidulile kuelekea kwa Nyonganyoga ambalo limebomolewa na mvua kubwa iliyonyesha jana

 eneo la daraja lililo bomoka
wasafiri wanao elekea Njombe wakitokea Ludewa mjini wakiangalia Daraja lililo bomoka na kushindwa kupita na magari yao

mwandishi wa mtandao huu na baadhi ya waandishi wa Radio best fm wakishuhudia  maafa hayo

Mvua kubwa zinazo endelea kunyesha wilayani Ludewa zimeendelea kuharibu miundo mbinu ya barabara  hasa ubomoaji wa madaraja ikiwa mpaka sasa ni madaraja manne tayari yameshaharibiwa,madaraja hayo ni mojawapo ya daraja la Ludewa magereza ambalo ni muhimu sana linalotumika na wananchi wa wilaya ya Ludewa kuelekea mkoani Njombe.

madaraja mengine ni daraja la kipulilo linalo unganisha kijiji cha Mbongo na Igalu katika kata ya manda jingine ni daraja la Kiyogo ambalo linaunganisha kijiji cha kiyogo na kingole ambalo lilikuwa katika hatua nzuri ya ujenzi,pia daraja la maboga linalounganisha kijiji cha Maholong'wa na kijiji cha Amani.

@ habari ludewa blog



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: