MBUNGE WA JIMBO LA LUDEWA MH.DEO NGALAWA AFANYIWA MAOMBI MAALUM ATOA BATI 4200 UJENZI WA VITUO VYA AFYA



 Mh.Deo Ngalawa akiongea na waumini wa kanisa la Anglikana mara baada ya maombezi

 Mh.Deo Ngalawa akiongea na waumini wa kanisa la Anglikana mara baada ya maombezi
 Mh.Deo Ngalawa na viongozi wengine wakifanyiwa maombezi
 hizi ni baadhi ya bati alizozitoa Mh.Ngalawa
Mh.Ngalawa akikabidhi bati wa madiwani wa wilaya ya Ludewa

 Mh.Ngalawa akiongea na baadhi ya madiwani

Mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Ngalawa amefanyiwa maombi maalumu ni kumpa nguvu ya kutenda kazi kwa bidii na bila uoga,maombi hayo yalifanywa hivi karibuni katika kanisa Anglikana mtaa wa Ludewa kijijiji .

katika maombi hayo ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali Mh.Ngalawa alisema kuwa anawashukuru wananchi kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kuwatumika kwani mchakato ulikuwa ni mgumu lakini kupitia maombi ya wapenda maendeleo aliweza kuibuka mshindi katika uchaguzi wa jimbo la Ludewa.

Mh.Ngalawa alisema kuwa ameanza kazi rasmi kwa kasi kubwa kwani alipoingia madarakani amevikuta vituo vitatu tu vya afya hali inayomfanya kufikiria kuwa na vingine kumi ambayo tayari ameshatoa bati za ujenzi wa vituo hivyo na ukarabati wa zahanati pamoja na nyumba za waganga ili kurahisisha huduma ya Afya kwa wananchi wa wilaya ya Ludewa.

kuhusu miundimbinu  Mh.Ngalawa alisema kuwa tayari kilometa 50 zinaanza kujengwa kwa lami ambazo aliziombea mtangulizi wake hivyo kwa kupitia ilani ya chama cha mapinduzi ya miaka mitano anaamini barabara ya Itoni, Ludewa, manda itajengwa kwa kiwango cha lami na kuwarahisishia wananchi katika usafiri.
 mwisho.




Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: