Manchester United 3-2 Arsenal: Mambo manne tuliyojifunza
- Louis Va Gaal aigiza kujirusha Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal ni mara chache sana kumuona kaachia kiti chake na kushuka kwenye touchline lakini jana aliona ni muhimu kwake kushuka na kuigiza kujiangusha kwa Lexis Sanchez.
Winga huyo kutoka Chile alikuwa kwenye kiwango cha juu mwanzoni mwa msimu huu akifanikiwa kufumania nyavu mara 10 katika michezo 25 kabla hajapata majeruhi.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 27 alikuwa pia na kiwango kibovu dhidi ya klabu yake ya zamani ya FC Barcelona katikati mwa juma lililopita katika mchezo wa Ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Beki wa pembeni wa Manchester United Valera aliyesajiliwa na aliyekuwa kocha wa United David Moyes alifanikiwa kumdhibiti Sanchez na kumfanya aonekane hana msaada kwa mechi nzima.
Mesut Ozil alifanikiwa kufunga goli moja na kupika jingine ambalo lilifungwa na Danny Welbeck na hivyo kuwafanya Arsenal kuwa na matumaini tena katika mchezo wa jana.
Ozil amekuwa kiungo muhimu katika safu ya ushambuliaji ya Arsenal toka alipojiunga na klabu hiyo akitokea Real Madrid kwa ada ya pauni milioni 42.5
Ozil amepika pasi 18 za magoli msimu huu zaidi ya mchezaji mwingine yeyote yule katika ligi kuu ya Uingereza na amefanya hivyo katika michezo 16 ya EPL.
Rashford mwenye umri wa miaka 18 amevunja rekodi ya kuwa mchezaji mdogo kuliko wote kufunga goli katika mechi yake ya kwanza akiwa na Mancheter United.
Kinda huyo aliyezaliwa katika jiji la Manchester alifunga magoli mawili na jingine likifungwa na Ander Herrera na kuwafanya Man united kuibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Arsenal.
Akiwa na umri wa miaka 18 na siku 157 James Wilson ndiyo alikuwa kinda wa Manchester United aliyekuwa anashikilia rekodi ya kufunga goli akiwa na umri mdogo zaidi.
Lakini Rashford amefanikiwa kufanya hivyo katika umri wa miaka 18 na siku 117. Rashford pia amekuwa kinda wa kwanza kufunga goli katika mashindano ya Ulaya tangu enzi za George Best alivyofanya hivyo October mwaka 1964.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment