Hatimaye PSG wasimamishwa Ligue 1 – Washindwa kuifikia rekodi ya Nantes




Waingereza wana msemo wao unaosema – (‘All the goods things come to an end’ – ‘Kila Jambo zuri hufikia mwishoni.’
  Msemo huu unaendana na kilichotokea usiku wa tarehe 28/2/2016 – Lyon waliwashangaza Paris Saint-Germain kwa kipigo cha 2-1 na kusitisha safari ya mabingwa watetezi kumaliza ligi bila kufungwa.
  Kinda wa Lyon Maxwell Cornet aliwapa uongozi wa mechi vijana wa Bruno Genesio mwanzoni mwa mchezo kabla ya Segie Darder kuongeza la pili na kuipeleka Lyon mapumziko wakiwa mbele 2-0.
  Lucas Moura alifanikiwa kurudisha goli moja lakini Lyon walikaza na kufanikiwa kupata ushindi ambao uliwaingiza kwenye Top 3 ya Ligue 1.
Matokeo hayo yamehitimisha rekodi ya PSG kutokufungwa katika mechi 36 katika Ligue 1 – rekodi iliyoanzia msimu uliopita, mechi yao ya mwisho kufungwa ilikuwa dhidi ya Bordeaux – walipofungwa 3-2.
  Rekodi ya kucheza mechi nyingi bila kufungwa kwenye Ligue 1 ndani ya msimu inashikwa na Nantes, mechi 32, rekodi hii waliweka msimu wa 1995/95. PSG wameishia mechi 27 bila kupoteza msimu huu


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: