Baada ya taarifa kutoka wiki iliyopita kupitia mitandao mbalimbali ya habari Duniani kote kuwa Kocha wa zamani wa FC Barcelona Pep Guardiola ambaye kwa sasa anainoa miamba ya soka nchini Ujerumani FC Bayern Munchen kuwa atajiunga na Manchester City habari inayoshika vichwa vya habari kwa sasa ni uwezekano wa kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho kujiunga na mashetani wekundu Manchester United.
Jose Mourinho na Pep Guardiola wanasemwa kuwa moja ya makocha bora Duniani lakini pia wakiwa wamejipatia mafanikio makubwa kwa miaka ya hivi karibuni katika vilabu vyao mbalimbali walivyofanyia kazi.
Lakini ikumbukwe Mourinho na Guardiola wamekuwa makocha wenye uhasama mkubwa katika kazi tangu wawili hao walipokuwa wakizinoa klabu kubwa za La Liga Real Madrid na FC Barcelona kwa pamoja.
Kama taratibu zitakamilika na Mourinho akajiunga na Manchester United basi tutashuhudia moja ya Upinzani mkubwa sana kuwahi kutokea katika ligi kuu ya nchini Uingereza kutoka na hitoria ya upinzani kati ya Mreno huyo na Mhisipaniola toka wakiwa La Liga.
Kwa Pamoja Mourinho na Guardiola wakiwa La Liga wamekutana mara 16 huku Mourinho akishinda mara 3 Guardiola akishinda mara 7 na sare mara tano.
Lakini kinachofurahisha na ambacho mashabiki wengi wanasubiri kuona ni kwamba Guardioloa anakuja katika Ligi kuu ya Uingereza inayotajwa kuwa Ligi yenye ushindani mkubwa kuliko Ligi zote Duniani ligi ambayo Jose Mourinho ameshachukua makombe matatu ya Ligi kuu nchini akiwa na klabu ya Chelsea.
Mashabiki wengi wa soka wanasubiri kuona je Guardiola ataweza kuimudu Ligi hiyo ambayo matokeo ya mwisho hayatabiriki ukizingatia pia kuwa Guardiola ana rekodi mbovu dhidi ya timu ya Uingereza katiuka ardhi ya Uingereza ambapo tayari mpaka sasa ameshacheza mechi 10 amefungwa mechi 4 ameshinda mechi 3 na ametoka sare mechi 3
Endapo Mourinho kocha mwenye mbwembwe nyingi maarufu kama The Special One atatua ngome Kongwe (Old Trafford) ni jambo la muda tu kusubiri na kuona nini kitatokea, Lakini Guardiola anatambua kuwa ana kibarua kizito sana kuishi kwa sifa zake katika ligi kuu ya Nchini Uingereza.
Comments
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment