Eden Hazard amekiri kwamba alituma ujumbe wa kuomba msamaha na kumpa pole Mourinho baadaya kufukuzwa kunako klabu ya Chelsea mwezi Desemba mwaka jana.
Kwa mujibu wa Hazard, kiwango chake kibovu ndiyo sababu kubwa ya kufanya hivyo, kwa sababu anadhani kuwa alikuwa ni mhanga wa kocha huyo kufukuzwa.
“Nilimtumia ujumbe wa kumuomba msamaha, ndiyo nilisikitishwa sana,” Hazard aliliambia The Guardian. “Tulifurahi kwa pamoja mafanikio ya msimu uliopita, lakini muda huu hatupo naye tena.
“Nilijihisi ni mwenye makosa makubwa sana kwa sababu msimu uliopita nilikuwa ni moja ya wachezaji waliokuwa na mchango mkubwa sana, lakini haikuwa hivyo msimu huu”.
“Sijawa katika kiwango bora msimu huu. Hivyo nilituma ujumbe kwa Jose na alikuja kwangu na kunitakia mafanikio mema. Kwa timu ambayo ilikuwa ni bingwa, halafu kuwa na matokeo ambayo tumekuwa tukiyapata msimu huu, ni jambo lisiloelezeka kabisa”.
“Mambo yameanza kuwa mazuri hivi karibuni, lakini bado hatuna matokeo ya ushindi kama tulivyozoea. Hakuna mtu wa kumnyooshea kidole kwa kilichotokea ndani ya Chelsea.”
Kwa pamoja Eden Hazard, Diego Costa na Cesc Fabregas ‘Soller’ walishutumiwa na mashabiki wa Chelsea kuwa ndiyo waliokuwa vinara wa kusababisha Mourinho afukuzwe Darajani kwa kucheza chini ya kiwango kitendo kilichopelekea klabui hiyo kupoteza michezo 9 kati ya michezo 16 ya mwanzoi ya Ligi kuu nchini England.
Kwa sasa Chelsea wanashika nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi kuu Nchini Uingereza na mpaka sasa Winga huyo kutoka Ubelgiji hajafunga goli hata moja katika Ligi kuu ya Nchini Uingereza, Mchezo unaofuata ni Kesho kati ya Chelsea na Manchester United ambapo Hazard anatarajiwa kuisaidia klabu yake kukwea katika msimamo wa Ligi kuu Nchini Uingereza.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment