JKT Ruvu imekubali kichapo cha magoli 4-0 kutoka kwa Yanga na kuirejesha timu hiyo kwenye reli baada ya kuwa na wiki ya tabu kufuatia kupoteza mechi yake ya kwanza kwenye msimu huu kwa goli 1-0 dhidi ya Coastal Union kabla ya kubanwa na kulazimishwa sare ya kufungana bao 2-2 na Tanzania Prisons mkoani Mbeya.
Simon Msuva amefunga magoli mawili kwenye mchezo huku Issoufou Boubacar akifunga goli lake la kwanza kwenye ligi tangu ajiunge na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili mwezi January na mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Donald Ngoma aweka goli moja kambani kukamilisha ushindi wa bao nne.
JKT Ruvu wameonekana kucheza vizuri kwenye mchezo wa leo lakini walizidiwa mbinu za kimchezo na Yanga ambao walikuwa wanatumia sana wachezaji wao wa pembeni (Msuva na Kaseke) katika mashambulizi yao mengi.
Ushindi huo unaipa Yanga faida ya kuendelea kubakia kileleni mwa ligi wakiwa wamefikisha jumla ya pointi 43 baada ya kucheza michezo 18 wakifuatiwa na Simba ambao wanapointi 42 wakati nafasi ya tatu ikiwa mikononi mwa Azam yenye pointi 42 sawa na Simba lakini inafaida ya michezo miwili mkononi kutokana na kwenda Zambia kucheza mechi za kirafiki.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment