ASKARI ANUSURIKA KIFO KWA KUPIGWA VIRUNGU NA ASKARI MWENZAKE KITUONI. WANANCHI WAMLALAMIKIA OCD KWA KUMLEA ASKARI HUYO.

 ASKARI ANUSURIKA KIFO KWA KUPIGWA VIRUNGU NA ASKARI MWENZAKE KITUONI. WANANCHI WAMLALAMIKIA OCD KWA KUMLEA ASKARI HUYO.


,Atenguliwa mkono,mguu na mbavu,simu zake zaharibiwa vibaya.

ASKARI wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU cha ukonga jijini Dar es salaam aliyejulikana kwa jina la Pc Bruno amenusurika kifo jana baada ya kupigwa vibaya kwa kutumia virungu na askari mwenzake wa kituo kikuu cha polisi mjini Ludewa katika Mkoa wa Njombe.

Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Bw Temu akihojiwa leo alishindwa kuthibitisha tukio hilo na kuahidi kufuatilia na kutoa majibu baadaye ingawa Awali alidai kupewa taarifa na Mkuu wa polisi wilaya OCD Emanuel Gariyamoshi kuwa hakuna taarifa yoyote ya kupigwa mtu.

Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo wanasema mhanga wa tukio pc Bruno alikutwa na majanga hayo akikaribia kufika katika kituo cha polisi alipokwenda kuelewa nini lilitokea kutokuelewana kati yake na mtangaji mmoja wa kituo cha radio kilichopo mjini Ludewa.

"" jamani askari Steven ambaye ni driver wa gari la ocd tumemwona akitokea ndani ya kituo cha polisi huku akiwa na rungu kubwa mkononi ambapo alimfuata Bruno wakaanza kumpiga na kuanguka kiraji na mwembe huku akilalamika maumivu huku akijitambulisha kuwa wamwache afike kituoni kwa vile nayeye pia ni askari mwenzao lakini hakusikilizwa "" walilaumu mashuhuda hao

Hata hivyo mmiliki wa Grocery ya Ruhuji Bi Magreti alikiri kutokea mabishano ya kutoelewana kati ya Wateja wake wawili yaani pc Bruno na mtangaji wa kike wa radio bestfm jambo lililopekea washikane na aliposhindwa kuamuria ugomvi huo alienda kuomba
msaada ktk kituo cha polisi kilichopo umbali wa mita100 tu, walipofika askari hao walimkuta mwenzao akiwa amechaniwa shati akatoa hela kununua shati lingine na kuelekea kituoni na kumwacha yule Dada hapa ndani.

 Wananchi mjini hapa wamelalamikia vitendo vya ukatili visivyo vya kibinadamu  vinavyofanywa na askari Huyo wa USALAMA barabarani PC STEVEN ambaye pia ni driver wa Ocd kwamba amekuwa akitangaza ubabe na vitendo vichafu lakini Mkuu wa polisi Emanuel Galiyamoshi anamtetea kwa sababu anayomaslahi maslahi na vitendo hivyo.

Nao madriver na waendesha bodaboda katika nyakati tofauti wamesema wamekutwa wakipigwa nakuonewa kila wakati na askari Steven humu Mkuu wake akifurahia wanashindwa sasa wapeleke malalamiko yao wapi.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: