Jamaa mmoja aliyejulikana kwa jina la Athumani mkazi wa Keko Mwanga, jijini Dar amenaswa akichana wavu wa dirisha la nyumba moja mtaani hapo na kushushiwa kipigo cha kufa mtu hali iliyomfanya ajitetee na kudai kuwa alikuwa akichana wavu huo kwa ajili ya kupiga chabo na si wizi kama alivyohisiwa.
Akizungumza baada ya wakazi hao kumweka chini ya ulinzi, Athumani alidai kuwa kila mara akiwa anapita karibu na dirisha la nyumba hiyo husikia sauti za mahaba ambapo siku hiyo alishindwa kujizuia na kutaka kuchungulia mchezo mzima ndipo alipofumwa na kupigwa.
Watu hao wenye hasira walipompekua walihakikisha kuwa siyo mwizi kwa kuwa hakuwa na vifaa vya kuibia dirishani na kumwacha akiondoka huku mwenyewe akiwa haamini kama kweli ametoka salama
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment