Inakuwa nini sasa masela? Kama vepe kitaani ni mpango mzima. Mambo ya mboyoyo mingi tupa kule. Ebana welikamu kwa sana kwenye mastori yetu ya ubaoni. Ndo kama hivo jeshi la mtu mmoko nipo ubaoni rede kwa kuwapa skonga la kitaa. Si ndo hivo chama langu? Basi kaa huku wewe tulisongeshe.
Siyo sekreti washkaji zangu laifu linakwenda resi kinoma hadi samu taimu wana wanataka kukata kitu cha pumzi bati hakuna kulala hadi kieleweke wanyama wangu.
Nani anabisha kuwa mtu mzima prezidaa amezima mbwembe na nyodo za wala bata kwa fasi ya viwanja? Wanangu wanaomaindi kitonga sasa ni fulu kwikwi. Hakuna mambo ya kuweka heshima tauni sasa hivi kozi dizaini kama mabomba hayatoi tena maziwa kama zamani. Unaambiwa sasa ni kitu cha wota tu tena wota lenyewe la maji ya chumvi.
Ngoja niwagonge na stori la watu fedenge ambao tumehaso wote kitambo bati wakalamba mashavu kwenye vitengo nyeti. Mazee unaambiwa wana walipomaliza tu kitu cha koleji walipita mlango wa baki wakazama kwenye manoti mengi ndani ya gavamenti.
Nawu huyo mwanangu mwenyewe wa kutumbua majipu alipotimba waiti hausi hapo Magogoni, kitumbua kimeingia mchanga laivu arifu.
Makachaa walikuwa wanagonga bata ndefu kitaa kama hawana akili freshi. Jamaa walikuwa wanawaona washkaji zao kama wamepoteza f’lani hivi so wakawa wanawafungia tu vioo kisha kuwarushia matope na kuwatimulia vumbi.
Masela walikuwa wanachenji mandinga na mabebiz wakare kama nguo mazee. Ilikuwa wakifika kiwanja wanajitoa fahamu arifu na kilichofuata ilikuwa ni bata mwanzo mwisho hadi majogoo. Si unajua zile za mapopoo? Ni mwendo wa mupe, muruke na kama kuna jembe aliyezama na hela ya ngama aliishia tu kula kwa macho.
Mwanangu mmoko ambaye alikuwa na mafyucha kwa mbali, akawa amepiga bingo na kuangusha bonge la kiota hapo kwa fasi ya Makongo. Sasa bana wakati mambo ya maujenzi yanaendelea si ndo kimfereji kimekata? Dah! Unaambiwa sasa hivi msela anagongea tu fegi kwa kitaa na hakuna dalili ya kumalizia mjengo umeishia madirishani.
Wale masela aliokuwa akiwatimulia vumbi nao wamemfungia vioo. Sasa anasafaje makachala wangu? Ebana zile mbwembwe na nyodo kwisha kabisa na kilichobaki ni fulu heshima. Mwana amenyookaje sasa? Mazee ni fulu kwere kitaa. Wana wanasema dhenki yuu prezidaa kwa kuleta usawa kwa kitaa.
Oyo masela nadhani nimesomeka! Mabovu yanapokutembelea masti uwe na heshima kwa wana kozi huwezi kujua tudei ni kwako dheni tumoro kwa mwana mwingine. Najikataa shaaa
Ludewa yetu na maendeleo yetu
About Rafiki Fm Ludewa
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment