WAKIMATAIFA YANGA VS AZAM ZAIDI YA PAMBANO LA MASUMBWI PALE ZANZIBARI


Wachezaji wa Azam FC na Yanga SC katika 'timbwili' wakati wa mchezo wao wa Mapinduzi Cup
Wachezaji wa Azam FC na Yanga SC katika ‘timbwili’ wakati wa mchezo wao wa Mapinduzi Cup
Bado burudani ya soka ipo Zanzibar kwa kuendelea kuchezwa michezo ya Kombe laMapinduzi, baada ya kupigwa mchezo wa tatu wa Kundi B mchana wa January 5 kwa kuzikutanisha timu za Mafunzo ya Zanzibar na Mtibwa Sugar ya Morogoro na mchezo kumalizika kwa Mtibwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Usiku wa January 5 ulichezwa mchezo wa nne wa Kundi B kwa kuzikutanisha timu zaAzam FC dhidi ya Yanga ambapo timu hizo zote zinachuana kwa karibu kutaka nafasi ya kuongoza katika Ligi Kuu Tanzania Bara, ila kisasi kikahamia katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi, haukuwa rahisi na ulikuwa wa kukamia kwa nahodha wa Azam FC John Bocco na beki wa Yanga Kelvin Yondani, kitendo ambacho kilipelekea John Boccokuoneshwa kadi nyekundu.

Hata hivyo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya goli 1-1, baada ya Azam FC kufunga goli la uongozi kupitia kwa Kipre Tchetche dakika ya 58, Yanga walikuja juu na kuongeza mashambulizi ila mabadiliko ya kuingia kwa beki wake wa kimataifa wa Togo Vicent Bossou kulizaa matunda baada kufanikiwa kuisawazishia Yanga goli dakika ya 83.

Sare hiyo imeenda kubadilisha msimamo wa Kundi B, sasa Yanga atakuwa  kileleni akiwa na point 6, akifuatiwa na Mtibwa Sugar wenye point nne, Azam FC wenye point 2 naMafunzo wakishika mkia kwa kuwa hawana point hata moja, Azam FC atacheza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mafunzo na Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar.



Pambano la Yanga vs Azam FC limemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1 lakini badala ya timu hizo kucheza mpira na kuonesha burudani kwa mashabiki waliofururika kushuhudia mchezo huo, badala yake mchezo huo ukageuka kuwa ulingo wa masumbwi.
Kipre Tchetche alianza kuifungia Azam FC bao la kuongoza lakini bao hilo halikudumu kwa dakika 90 kwani Vincent Bosou alisawazisha bao kwa upande wa Yanga ambalo nalo lilizua utata huku wachezaji wa Azam wakipinga maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo kulikubali goli hilo.


Taarifa zaidi inakujia hivi punde


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: