Wahariri wa Mawio wajisalimisha Polisi

Dennis Mwalongo


Wahariri wa gazeti la Mawio waliokuwa wanatufutwa na Jeshi la Polisi, jana mchana walikwenda Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa.  
Wahariri hao walihojiwa kwa muda wa saa nne kuanzia saa 8:59 mchana hadi Saa 12 : 40 jioni. Wahariri hao ni Jabir Idrisa na Saimon Mkina ambaye aliongozana na Frederick Kihwelo, 
ambaye ni mwawanasheria wa gazeti hilo, Absalom Kibanda (mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri), Saed Kubenea (mkurugenzi wa kampuni ya Halihalisi Publishers) na Ansbert Ngurumo, aliyekuwa mhariri mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima. 

Januari 15, kamanda polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwataka wahariri hao kujisalimisha kituoni hapo, akidai kuwa wameandika habari za uchochezi. Mapema jana kabla ya kuwasili kwa wahariri wa gazeti hilo, Kamanda Sirro alidai kuwa wamekuwa wakiwatafuta bila ya mafanikio. Wakati Idrisa anaingia ofisi ya Kamanda Sirro kwa ajili ya mahojiano, waandishi walizuiwa, waliambiwa hawahusiki, baadaye saa 9:15 alasiri Mkina aliwasili na kwenda moja kwa moja kwenye ofisi hiyo, lakini alitakiwa asubiri nje. “Sisi jukwaa la wahariri hatutakubali kufanya kazi na waziri wa aina hii na tutatoa tamko ngojeeni,”alisema Kibanda baada ya kufika kituoni hapo. Kwa upande wake Kubenea alisema alifika hapo kwa sababu miongoni mwa walioshikiliwa na polisi ni mfanyakazi wake.


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: