Kocha Kim afungua milango ya kufanya kazi na TFF upya


Dennis Mwalongo


Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Kim Poulsen  
Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Kim Poulsen amefunguka juu ya uwezekano wake wa kufanya kazi nchini akisema kwa sasa hana kizuizi chochote endapo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litampa majukumu ya kufanya. 

Kim alisema kwa sasa yuko nchini kwa mapumziko mafupi, lakini katika taaluma yake hana kibarua chochote na yuko tayari kulitumikia Taifa la Tanzania kwa mara nyingine. Kim alisema katika mapumziko yake amekuwa akipata muda wa kuangalia mechi za Ligi Kuu Bara na amefurahi kuona katika kazi ya mwaka mmoja aliyoifanya awali katika kuzalisha vipaji wako vijana wanaozichezea timu kubwa za Simba, Yanga na Azam, 
hatua ambayo kwake imempa picha kwamba Tanzania kuna vipaji vya kutosha. Kocha huyo alisema katika mkutano wake na Rais wa TFF, Jamal Malinzi kiongozi huyo alionyesha nia ya kutaka kuwekeza zaidi katika soka la vijana, jambo ambalo endapo atampa jukumu hilo yupo tayari kulifanya. “Nilipoondoka hapa Fifa walinihitaji kufanya nao kazi,
 lakini kuna mambo hayakuwa sawa na baadaye Rwanda wakanihitaji, nilihitaji muda kutafakari jukumu walilotaka kunipa kwangu, ni bora nikafanya kazi hapa Tanzania, ambako nakujua na kuna msingi wa kianzio kuliko sehemu nyingine,” alisema Kim.



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: