Kikosi cha Majimaji kinachosimamiwa na Hassan Banyai kimeendelea kuwa na matokeo mabaya katika mechi za ligi kuu na sasa katika mashindano ya kombe la FA, na katika mchezo huu timu ya Majimaji imechezesha kikosi B wakati wachezaji wa kikosi cha kwanza wakigoma kuingia uwanjani wakidai kutolipwa stahiki zao hali inayozidi kuwa katisha tamaa mashabiki wa mabingwa hao wa zamani wa ligi ya Tanzania bara.
Ni mchezo uliokosa ladha kutokana na mvua iliyonyesha kwa saa kadhaa na mpaka kipindi chote cha dakika 90 za mcheo huo na kufanya uwanja wa Majimaji kuwa na maji kiasi cha kufanya mchezo huo kukosa ufundi kabisa.
Lakini bahati imeendelea kuwa mbaya kwa ‘Wanalizombe’ baada ya kukubali kichapo cha cha magoli 2-1 kutoka kwa majirani zao JKT Mlale. Magoli ya JKT Mlale yamefungwa katika dakika ya 10 kupitia kwa Rafael Siame na dakika 23 Richrd Mwandiga akaiandikia timu yake yaJKT Malale goli la pili na goli la kufutia machozi la Majimaji likafungwa na Alex Nzari katika dakika ya 48 kipindi cha pili na kwa matokeo haya Majimaji inakufulumushwa nje ya mashindano ya kombe la shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup.
Mpaka sasa huenda timu ikashindwa kusafiri kesho kuelekea Tanga kwa ajili mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara wakati viongozi wanajaribu kutafuta suluhu ili mambo yaende barabara clubuni hapo.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment