HENRY JOSEPH: HIVI NI VITU AMBAVYO SAMATTA ATAKUTANA NAVYO ULAYA, ANATAKIWA KUWA MVUMILIVU


Henry Joseph Shindika
Mchezaji wa muda mrefu wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Simba Henry Joseph Shindika ambaye kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, ametoa ushauri kwa nyota wa soka la Tanzania na Afrika Mbwana Samatta ambaye hivi karibuni atatimka Ulaya kwenda kukipiga kwenye klabu ya Genk ya nchini Ubeligiji.
Henry ambaye ameshawahi kuchea soka la kulipwa barani Ulaya kwenye klabu ya Kongsvinger ya nchini Norway amesema, Samatta anatakiwa kuwa mvumilivu pindi atakapofika Ulaya kwasababu kuna vitu vingi atakavyokutananavyo ambavyo vitakuwa vigeni kwake na vya tofauti na Afrika.
Kiungo huyo mzoefu hakuacha kumpongeza Samatta kwa hatua aliyopiga ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani siku chache zilizopita huku akisisitiza kuwa Samatta amaeitangaza vizuri Tanzania.
Henry Joseph wakati akizungumza na mwandishi wa mtandao huu
Henry Joseph wakati akizungumza na mwandishi wa mtandao huu
Shaffihdauda.co.tz imepiga story na Henry Joseph ambaye kwa sasa yupo visiwani Zanzibar akiwa na timu yake ya Mtibwa Sugar inayosuburi kucheza mchezo wa fainali ya Mapinduzi Cup dhidi ua URA ya Uganda leo Jumatano January 13, 2016.
“Kwanza nampa hongera kwa alipofikia ni hatua kubwa na ameiwakilisha nchi yetu, kitu nachotaka kumshauri ni kwamba, sasa anaenda kwenye nchi za watu, cha muhimu ni kuwa na uvumilivu kwasababu wenzetu wanavyoishi ni tofauti na Afrika kwahiyo uvumilivu ndiyo kitu muhimu kwasababu anaweza kujikuta anaishi pekeyake”, amesema Henry Joseph ambaye ni mzoefu wa soka la Tanzania lakini pia akiwa amewahi kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
“Wakati mwingine huwa wanamambo ya jabu-ajabu kwahiyo anatakiwa awe mvumilivu pia na azoee, achukulie kule amekwenda kufanya kazi na afanye kazi”.
Henry Joseph akionesha namba ya jezi yake ambayo hakuwa tayari kusema mara moja namba hiyo inamaana gani kwake
Henry Joseph akionesha namba ya jezi yake ambayo hakuwa tayari kusema mara moja namba hiyo inamaana gani kwake
“Kingine ni ubaguzi, lakini kitu cha muhimu ni yeye kujua nini kilichompeleka. Afanye kazi, aongeze kiwango chake hawezi kujua pale hawezi kukaa milele. Mwaka mmoja au miwili anaweza kuondoka kwenda sehemu nyingine kwahiyo huko kwine pia anaweza kukutana na changamoto hizohizo kwahiyo cha muhimu awe na moyo wa uvumilivu kwa chochote atakachokikuta kule”.
“Atakutana na wenzake atakuwa anawauliza namna mambo yanavyokwenda watakuwa wanamwambia, atakutana na kitu kinaitwa ‘boredness’ hasa anaporudi nyumbani kwasababu ameshazoea akirudi anakutana na washkaji anaongea na Ulimwengu kwahiyo hali hiyo anatakiwa aijue. Muda mwingine atakuwa anajikuta peke yake ndani, hivyo ni baadhi ya vitu ambavyo atarajie kukutana navyo siku za mwanzo kabisa”.
“Maisha ya kule siyo kila siku unatoka unaenda kwa washkaji, halafu hakuna mambo ya kambi kule kukaa pamoja kwa muda mrefu, kila mtu anakaa kwake mnakutana mazoezini na siku ya mechi. Kama kunasafari mechi za away unapangwa muda wa kukutana kwa ajili ya safari. Kwahiyo yale mazoea ya kusema natoka naenda kwa flani yanakuwepo lakini siyo mara kwa mara”.
Hii hapa sauti ya Henry Joseph akitoa ushauri wake kwa Mbwana Samatta kuhusu maisha ya soka la Ulaya




Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: