Mapinduzi Cup: Simba yavuliwa ubingwa na Mtibwa, fainali Mtibwa vs URA, Januari 13
Nusu fainali ya Kombe ya Mapinduzi ilifanyika jana kwa michezo miwili kupingwa ambapo nusu fainali ya kwanza ilikuwa kati ya Simba na Mtibwa Sugar na nusu fainali ya pili ikawa kati ya Yanga na URA ya Uganda.
Mchezo wa nusu fainali ya kwanza ulimalizika kwa Mtibwa kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila, goli lililofungwa na kiungo wa timu hiyo, Ibrahim Rajab katika dakika ya 45 ya mchezo huo.
Baada ya kipigo hicho, rasmi Simba SC inakuwa imevuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na Mtibwa Sugar.
Nao wapinzani wa jadi za Simba, Dar Young African walitolewa katika mashindano hayo ya URA ya Uganda katika hatua ya mikwaju ya penati 4 kwa 3 baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja.
Goli la Yanga katika mchezo huo lilifungwa na Amisi Tambwe katika dakika ya 13 na baadae URA ilisawazisha goli katika dakika ya 76 kupitia kwa mchezaji wao Peter Lwasa na hadi dakika 90 zilipomalizika wakamaliza kwa sare na kuingia hatua ya penati.
Penati za Yanga zilifungwa na Kevin Yondani, Deo Munishi na Simon Msuva na Malimi Busungu na Geoffey Mwashiuya wakikosa, penati za URA Said Kyeyune, Deo Othieno, Jimmy Kulaba na Brian Bwete huku Sam Sekito akikosa.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment