…
Mchezo wa mwisho wa Kundi B katika michuano ya Kombe la Mapinduzi umepigwa usiku huu katika dimba la Amaan visiwani Zanzibar, huu ni mchezo ambao umezikutanisha timu za Mtibwa Sugar dhidi ya Dar Es Salaam Young African, licha ya kuwa Mtibwa naYanga wamefuzu hatua ya nusu fainali, haukuwa mchezo rahisi kwa timu zote mbili.
Kila timu ilionekana kusaka ushindi ili ipate nafasi ya kuongoza Kundi B nusu fainali ikutane na timu dhaifu ya Kundi A, yaani mshindi wa pili. Mtibwa walianza kwa kasi na dakika ya 10 Shiza Kichuya akafanikiwa kupachika goli nyavuni kwa shuti kali la nje ya 18, Yanga ambao walikuwa na kikosi makini.
Hawakuwa na papara licha ya kuwa walikuwa nyuma kwa goli moja kwa bila, hadi pale dakika ya 42 mshambuliaji wao wa kimataifa wa Niger Issofou Boubacar kupachika goli la kwanza. Yanga walizidi kuonesha dhamira ya kuhitaji ushindi katika mechi hii, licha ya kuwa tayari walikuwa wamefanikiwa kutinga nusu fainali.
Kocha wa Yanga Hans van Pluijm alifanya mabadiliko yaliozaa matunda kwa kumtoaAmissi Tambwe na kumuingiza Malimi Busungu aliyeenda kupachika goli la pili, na kuufanya mchezo umalizike kwa Yanga kuibuka wa goli 2-1. Kwa matokeo hayo Yangaanasubiri mshindi wa pili wa Kundi A kucheza nae hatua ya nusu fainali, wakati Mtibwa Sugar wakimsubiri mshindi wa kwanza wa Kundi A
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment