BODABODA WAKIWA KWENYE VITUO VYAO VYA KAZI WAKIWA WAMESUSIA KUPAKIA ASKALI WA POLISI KAMA ABIRIA
Wamiliki Na Madereva Wa Pikipiki Maarufu Kama Bodaboda Mjini Njombe Wametangaza Mgomo Wa Kutoawapakia Askali Polisi Kwa Madai Kuwa Wanawanyanyasa Pindi Wanapokuwa Barabarani.
Hatua Hiyo Inakuja Ikiwa Siku Chache Tangu Jeshi la Polisi Kuendesha Oparesheni Ambayo Wamedai Imewapa Athari za Kiuchumi Kutokana na Msimu Huu Kuwa Mgumu Kibiashara.
Aidha Wamesema Wamekuwa Wakiwanyanyasa Kwa Kuwakamata Kwa Kile Kinachodaiwa Wanakiuka Sheria Za Usalama Barabarani Kwa Kupanda Pikipiki Kama Abiria Na Wakifika Kituoni Wanawashikilia Kwa Makosa Hayo.
Operesheni Hiyo Ambayo Imezua Malalamiko Lukuki Miongoni Mwa Madereva Hao ni Pamoja na Ile Iliyolenga Kuwabaini Waharifu Na Wanaokiuka Kanuni Na Sheria Za Usalama Barabarani Kwa Kushindwa Kuvaa Kofia Ngumu,Kuendesha Pikipiki Bila Leseni Pamoja na Makosa Mbalimbali Kwa Madereva Kupitia Vyombo Vya Moto.
Wamiliki Na Madereva Hao Pia Wamelitupia Lawama Jeshi La Polisi Kupitia Kitengo Cha Usalama Barabarani Kwamba Wanaendesha Oparesheni Hiyo Pasipo Kutoa Elimu Na Amani Wakati Wa Kukamata Pikipiki Hizo Kwa Madai Wanakamatwa Hata Wale Wasio Na Makosa Na Kutafutiwa Makosa Ili Mradi Wakalipe Faini Ya Shilingi Elfu 30.
Filemon Mwinuka Ni Mwenyekiti Wa Madereva Pikipiki Ali Maarufu Kama Bodaboda Wilaya Ya Njombe Ambaye Amekiri Kuwepo Kwa Mgomo Wa Kutopakia Askari Polisi Yeyote Kuanzia Sasa Kwa Kile Kinachoelezwa Kuwa Utaratibu Wanaotumia Katika Uendeshaji Oparesheni Hiyo Unawaumiza Na Kuwakandamiza .
Kwa Upande Wake Mrakibu Mwandamizi Wa Polisi Mkoa Wa Njombe John Temu Amesema Oparesheni Hiyo Ya Ukamataji Wa Pikipiki Zinazotiliwa Shaka Pamoja Na Magari Inaendeshwa Kwa Mujibu Wa Sheria Nakwamba Zaidi Ya Shilingi Milioni 17 Zimepatikana Kutokana Na Tozo Za Makosa Mbalimbali.
Zaidi Ya Pikipiki Mia Nne Zimekamatwa Na Kutozwa Faini Za Makosa Mbalimbali Ya Usalama Barabarani Huku Magari Hamsini Nayo Yakikamatwa Na Kutozwa Faini Hizo Kwa Makosa Ya Kuzidisha Abiria ,Kutovaa Kofia Ngumu, Kutokuwa Na Leseni,Kuchanganya Abiria Na Mizigo Na Mwendokasi Wakiwa Barabarani.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment