Liverpool haionekani kuwa tayari kuwania nafasi nne za juu. Nguvu, uongozi na ari ya kujiamini imepotea katika klabu hiyo yenye maskani yake pale Anfield. Ikiwa inaendelea kupata matokeo yake ya kusuasua mapema ya leo katika mchezo wa mapema kabisa na wa kwanza kwa mwaka 2016 Liverpool imechapwa bao 2-0 dhidi ya West Ham.
Magoli ya Michail Antonio katika kipindi cha kwanza ambalo lilizua mjadala kwa kuonekana kama lilianzia mahali ambapo Antonio alimchezea rafu Alberto Moreno. Lakini Antonio ni wa kupongezwa kwani alikimbia takribani mita 90 mpaka anafunga goli hilo kwa kichwa krosi nzuri iliyopigwa na Ener Valencia huku mabeki wakizubaa.
Liverpool walimiliki mpira zaidi ila hawakuonekana kuwa na madhara. Mchezaji Christian Benteke ameendelea kuzua maswali kama ulikuwa usajili sahihi kwa klabu hiyo. Firmino pia anaonekana kuwa na homa za vipindi kwa kiwango chake kimekuwa cha kupanda na kushuka. Liverpool walimiliki mpira kwa asilimia 65, wakapata kona tisa, wakafanya mashambulizi 23 lakini 3 pekee yakilenga goli.
Wakati Liverpool wakijaribu kuweka mambo sawa katika kipindi cha pili, Mchezaji wao wa zamani Andy Carol akahitimisha sherehe kwa kufunga bao safi la kichwa huku kosa likionekana kuendelea kuwa lile lile la mabeki wa kati kuwaachia mzigo wa kuokoa mipira ya vichwa mabeki wa pembeni.
HIGHLIGHTS
https://www.youtube.com/watch?v=H6xRx2PUzmI
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment