EXCLUSIVE INTERVIEW: SAMATA AWEKA WAZI MIPANGO, MALENGO NA NDOTO ZAKE KUHUSU SOKA LA ULA


Samatta-JPN 7
Dili la Mbwana Samatta kujiunga na klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji limeshakamilika kwa asilimia nyingi, kilichobaki ni mchezaji huyo kujiunga na klabu hiyo na kuanza maisha mapya barani Ulaya baada ya kufanya makubwa kwenye soka la Afrika.
Samatta atajiunga na Genk hivi karibuni akitokea kwenye klabu yake ya TP Mazembe iliyompa mafanikio makubwa kwenye soka la Afrika ikiwa ni pamoja na kutwaa taji la klabu bingwa Afrika pamoja na kucheza michuano ya klabu bingwa duniani 2015 (FIFA Club World Cup) ambayo hushirikisha vilabu bingwa vya kila bara lakini vilevile kwasasa yupo kwenye majina matatu yaliyoingia kwenye fainali ya kuwania tuzo ya mchezaji bora Afrika anayecheza Afrika.
Mtandao huu umepiga story na Samatta kutaka kujua malengo, mipango na mikakati ya Samatta juu ya soka lake hasa baada ya kuwepo kwa taarifa zinazothibitisha mchezaji huyo anakwenda kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
Samatta amesema klabu ya Genk kwake ni kama njia tu ambayo anapita ili kutimiza ndoto zake ambapo amesema, siku zote ndoto yake ni kucheza katika klabu yoyote inayoshiriki ligi kuu ya England (EPL)
“Mimi binafsi ninafuraha na ninajivunia kwa nchi yangu na taifa langu kwasababu ni vitu ambavyo siku zote tulikuwa tunavitamani siku zote. Hata mimi wakati bado mdogo nilikuwa natamani kuwaona watu wamepata mafanikio wapo kwenye vilabu ambavyo kila siku tunaweza kuwaona”, alisema Samatta wakati alipozungumza na shaffihdauda.co.tz.
“Lakini nadhani Genk ni njia ambayo itanirahisishia kuwa katika mazingira ya Ulaya, sidhani kama naenda kusaini Genk halafu mwisho wa siku ndiyo basi kwasababu nilikuwa nina ndoto ya kwenda kucheza Ulaya. Genk naifanya kama njia ya kuniwezesha kuzoea mazingira ya Ulaya ili hata kama itakuwa imetokea kwenda kwenye klabu kubwa ambazo kila weekend watu wanakaa kuviangalia isiwe jambo geni tena”.
“Ulaya ni tofauti na Afrika, kule watu wanatumia opportunities kwa baiashara tofauti na Afrika unaweza ukawa unacheza lakini watu wakawa hawataki kukutumia kama biashara kwahiyo nadhani Genk itakuwa njia rahisi kunifanya mimi kama biashara. Genk ni klabu ambayo ina historia ya kuuza wachezaji ambao leo hii watamba kwenye vilabu vikubwa Ulaya”.
“Kwahiyo ilinivutia kiasi flani nifike Genk ili iwe njia rahisi kwangu kucheza vilabu vikubwa vya Ulaya kwasababu ndiyo ndoto ambazo kila siku naziota kwamba siku moja niwe kwenye klabu moja kubwa Ulaya ili kuwasaidia vijana wengine ambao wanania, wakiona mtu flani yuko sehemu flani inakuwa rahisi kwao kuwa na chachu”.

Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: