Ghasia za awali mjini Bujumbura.
Ghasia
zimeshudiwa usiku wa kuamkia Ijumaa katika kata mbali mbali za mji ya
Bujumbura, Burundi, ambapo milio ya risasi na milipuko mingine
imesababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine kumi na watatu.
Msemaji
wa polisi ameandika kwenye mtandao wake wa tweeter kuwa miongoni mwa
waliouwawa ni wahalifu wawili na raia wa kawaida mmoja. Haya yamejiri
wakati wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa walipokuwa
wakikamilisha ziara yao ya siku mbili nchini humo, ambapo Ijumaa jioni
walipokelewa na Rais Pierre Nkurunziza kwa mazungumzo katika mkoa ulio
kati kati mwa Burundi wa Gitega.
Awali,
wajumbe hao walikutana kwa mazungumzo na makamu wa kwanza wa rais
Gaston Sindimwo. Mara walipowasili Alhamisi usiku, wajumbe hao walipata
nafasi ya kukutana na marais wawili wa zamani wa Burundi.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment