Gianluigi Donnarumma
Gianluigi Donnarumma katika bora wake.

Dirisha la Januari la usajili vilabu vingi vimekuwa vikitumia kama sehemu ya kusajili wachezaji ili kuziba nafasi ambazo zinaonekana kuwa na mapungufu katika vikosi vya timu zao kama jinsi Man United inavyohusishwa usajiri wa baadhi ya wachezaji.
Mmoja wa wachezaji ambaye alikuwa akihusishwa na Man United ni golikipa anayechipukia wa AC Milan, Gianluigi Donnarumma ambaye ilikuwa ikisemekana kuwa Man United imepeleka ofa ya Pauni Milioni 30 ili kumsajili golikipa huyo.
Akizungumza na kituo cha tv cha RAI, Mkurugenzi Mtendaji wa AC Milan, Adriano Galliani amesema kuwa AC Mian haijapokea ofa yoyote kutoka kwa Man United na hata kama wakipeleka ofa hawana sababu ya kumuachia kinda huyo ambae ana miaka 16.
“Yupo na ataendelea kuwepo ni golikipa wa Milan,” alisema na Galliani na kuongeza “Hatujapokea ofa yoyote kumhusu yeye na hata kama ikija hatutaikubali”
Galliani ambaye mwezi ujao anataraji kufikisha miaka 17 ndiyo golikipa mdogo kuwahi kucheza katika michezo ya Ligi Kuu ya Italia na mpaka sasa ameshacheza michezo 11 ya Seria A pia anafananishwa kuja kuchukua nafasi ya Gianiluigi Buffon katika kikosi cha Italia.