Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limevifungia vilabu vya Hispania, Real Madrid na Atletico kutosajiri mchezaji yoyote kwa miaka miwili baada ya kuvunja kanuni za usajili wa wachezaji chini ya miaka 18.
Katika taarifa imeyotolewa na FIFA imesema kuwa timu hizo zinaweza kufanya usajiri kwa mwezi huu wa Januari kwenye dirisha dogo la usajiri baada ya hapo wataanza kutumikia adhabu ambayo wamepewa.
Taarifa hiyo imesema kuwa, usajili wowote ambao unamhusisha mchezaji ambaye ana miaka chini ya 18 una sheria zake ambazo ni pamoja na mchezaji anaweza kusajiriwa na klabu kama na wazazi wake wanahamia eneo ilipo klabu hiyo lakini kwa shughuli tofauti na soka, kama ni mchezaji kutoka nchi za Jumuiya ya Ulaya kwa mchezaji mwenye umri kati ya miaka 16-18 au kama anaishi ndani ya kilimota 100 kutoka ilipo klabu hiyo.
Real Madrid na Atletico Madrid sio klabu za kwanza za Hispania kukutana na adhabu hiyo kwani hata mwaka 2015 Barcelona ilifungiwa kutokusajiri mchezaji kwa kipindi cha mwaka mzima kwa kufanya usajiri bila kufuata kanuni na mchezaji kutokea Japan, Takefusa Kubo alirudishwa nchini kwao baada ya Barca kupewa adhabu hiyo.
Aidha baada ya kutoka kwa taarifa hiyo, Atletico Madrid tayari wametoa taarifa ya kumuongezea mkataba mchezaji wake, Antonie Griezmann mkataba wa miaka minne na nusu na sasa kupanda thamani hadi kufikia Pauni Milioni 75.5
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment