Nini Kinafuata Kwenye Maisha Ya C. Ronaldo: Umri Unamtupa Mkono, Vita ya vs Messi na Bale Zinaaza Kumshinda



Cristiano Ronaldo alishika nafasi ya pili kwa mara nyingine nyuma ya Lionel Messi katika FIFA Ballon d’Or na kwa namna inavyoonekana atahitaji kufanya mabadiliko makubwa katika career yake ili aweze kushinda au hata kubakia katika Top 3 ya wachezaji watakaogombea Ballon D’Or kuanzia msimu ujao. 
Pia kuna uwezekanao mkubwa akawa mchezaji wa pili ndani ya Real Madrid. Kurudi kwenye kiwango kwa Gareth Bale ambaye ni mdogo kwa Ronaldo kwa miaka 5 kunatoa picha hili linawezekana.
Huku tetesi za kwenda Paris Saint-Germain zikizidi kushika hatamu na pia kwenda kumalizia soka katika ligi ya Marekani – MLS, tuangalie options alizonazo nahodha huyu wa Ureno ambaye kashashinda kila kitu – ili aendelee kudumu kwenye soka la kiwango cha juu.
08353B9400000514-3397026-image-a-14_1452673376746Chaguo Namba 1: KUHAMIA PSG
Zlatan Ibrahimovic anakaribia kuondoka, Ronaldo atakuwa ataingia kwenye timu wakati muafaka. Atachukua majukumu commander-in-chief, kiongozi wa timu na atafanywa mfalme wa Paris huku akilamba mshahara mnono labda zaidi ya anaopata Santiago Bernabeu.
Changamoto mpya itakuwa kuiongoza PSG kutwaa ubingwa wa ulaya. Tayari ameshaanza kujifunza lugha ya kifaransa kama alivyosema mwenyewe katika usiku wa Ballon d’Or – ‘Naongea kidogo kifaransa – ‘comme ci, comme ca‘ aliongea Ronaldo.
Inafahamika kwamba anapatana vizuri na Laurent Blanc na pia Raisi wa klabu hiyo Nasser Al-Khelaifi. Inaweza kuwa kitu kisichoridhisha kama ataishia tu kushinda ubingwa wa Ligue 1, lakini fikiria kama ataiongoza klabu hiyo kushinda ubingwa wake wa Champions League? Kitaakuwa kitu kikubwa zaidi katika maisha yake ya soka.
Baada ya kuitumikia PSG kwa miaka miwili labda ndio anaweza kuamua kwenda MLS, Akitembea kifua mbele kwenda US huku akiacha legacy kubwa ndani ya jiji la Paris.
Uwezekano: 9/10
2FF6805C00000578-3397026-image-a-11_1452673216112Chaguo Namba 2: KUENDELEA KUBAKI MADRID KWA MIAKA 2, HALAFU AENDE MLS 
Hakuna anayeweza kumfanya Ronaldo aondoke Madrid. Ana mkataba mpaka 2018 na hata klabu isiyokuwa na aibu katika kuwaacha wachezaji kama Los Blancos hawatoweza kumuacha Ronaldo – mfungaji wao bora kabisa wa klabu katika historia ya timu hiyo. Wanaweza kuamua kuondokana na mzigo mzito wa mshahara wake na kupaa mfedha nyingi kwa kumuuza Ronaldo, lakini kama Ronaldo atataka kubaki basi anaweza kuendelea kubaki.
Faida ya kuendelea kubaki Spain ni kupata mataji zaidi, kwa sababu kwa hakika Real watashinda tu vikombe ndani ya misimu mitatu ijayo.
Jambo baya litakuwa ni kuanza kupoteza umuhimu ndani ya timu. Bale alionyesha kiwango cha juu mno wikiendi iliyopita – akiweka rekodi ya kuwa mfunga anayefunga kwa kichwa zaidi katika La Liga. Je Ronaldo atakuwa tayari kupoteza nafasi yake ndani ya timu – kutokuwa na uhakika na namba, kupunguziwa majukumu ya kupiga penati na adhabu ndogo?
Ronaldo anaweza kuendelea kuitumikia Madrid kwa misimu miwili na baada ya hapo akaelekea MLS, lakini atahitaji kufanya kazi ya zaida mno kurudisha kiwango cha juu ili kufanikiwa kufanya hivyo.
Kutokana na kifungo cha Madrid kutokusajili au kuuza mchezaji katika vipindi viwili vijavyo vya usajili – Ronaldo anaweza kufanya maamuzi katika dirisha hili au kusubiri mpaka wakati wa kiangazi 2017.
Uwezekano: 8/10
1875E60A000005DC-3397026-image-a-16_1452673604401Chaguo la 3: KUREJEA OLD TRAFFORD
Ed Woodward atakuwa kashawaza idadi ya jezi atakazouza siku itakapotangazwa Ronaldo amerejea. Fikiria nyimbo za ‘Viva Ronaldo’ zitakavyokuwa zikiimbwa katika mechi yake ya kwanza Old Trafford. Litakuwa jambo kubwa.
Lakini Ronaldo sio yule aliyeondoka mwaka 2009 na United sio klabu ile ile aliyoiacha. Inategemea ni kocha gani atakuwepo katika benchi la United wakati huo United itakapoamua kumsajili Ronaldo.
 Premier League itakuwa sehemu ngumu sana kwa Ronaldo kumalizia mpira, na heshima yake aliyojijengea inaweza kuwa hatarini kupotea. Je ni vyema kuacha kumbukumbu zibaki kama zilivyo? Real wanaweza kuwa wagumu kufanya biashara na United – labda iwepo biashara ya itakayomhusisha David De GEA. Lakini bado suala la kufungiwa kwa Madrid linaweka suala kwenye mashaka zaidi.
Uwezekano: 4/10
324923-cristiano-ronaldo-ancelottiChaguo 4: BIG SURPRISE – KWENDA BAYERN
Bayern Munich? Uhusiano mzuri wa Ronaldo na Carlo Ancelotti sio siri kabisa, alimpigia kura ya kuwa kocha bora wa mwaka hivi juzi katika Ballon D’or – watu hawa wawili walijenga mahusiano mazuri sana wakati Carlo alipokuwa kocha wa Madrid.
Inawezekana pia akaamua kwenda kumalizia mpira Ureno – Sporting Lisbon, maisha yake ya soka yalipoanzia. Mahala pengne ni China na Qatar.
Pia haitokuwa jambo baya kumuiga Beckham kwenda USA baada ya kumaliza mkataba wake.
Uwezekano: 2/10

@SHAFFI DAUDA



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: