IMwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) wilayani hapa Mkoa wa Mbeya, Denis Maria ametiwa mbaroni kwa madai ya kukiuka agizo la Serikali la kupiga marufuku mikusanyiko zikiwamo harusi ili kukabiliana kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu.
Denis alikamatwa juzi baada ya kuitisha mkutano wa vijana karibu 100 wa Chadema uliokuwa na lengo la kuwajadili viongozi wa chama chake wanaodaiwa kuvunja kufuli za ofisi za chama wilaya baada ya kufungwa na vijana hao.
Katibu Mwenezi wa Chadema, Donald Mwaisango alisema kiongozi huyo alikamatwa na polisi akiwa kwenye kikao.
Alisema baada ya kutoa maelezo aliwekewa dhamana na huenda leo akapelekwa mahakamani.
Mbali ya kumkamata kiongozi huyo, polisi walimkamata pia meneja wa ukumbi huo, Steven Minja kwa tuhuma za kuruhusu mikutano kufanyika wakati ilipigwa marufuku.
Mwishoni mwa mwaka jana, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Clemence Kasongo na Mkuu wa Wilaya, Thea Ntara walipiga marufuku mikusanyiko ya aina yoyote ile.
Ugonjwa huo uliikumba Wilaya ya Kyela na kusababisha watu 180 kuugua na wengine sita kufa.
CHANZO: MWANANCHI

Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment