MADOPE LUDEWA WALIA NA VYOO MAENEO YA BIASHARA






LUDEWA
Wananchi wa kijiji cha madope kitongoji cha njia panda wilayani ludewa Mkoani njombe wameiomba serikali kuweza kufuatilia hali ya usafi wamazingira kijijini hapo kwani kumekuwepo na hatari kubwa ya kuzuka  kwa magonjwa ya mlipuko kutokana na hali ya uchafu unao kizunguka kijiji hicho.

Akizungumza na mtandao huu moja kati ya mwananchi amesema kuwa wamekuwa wakipeleka malalamiko katika ofisi za kijiji kuhusiana na ukosefu wa vyoo katika maeneo ya kufanyia biashara lakini mpaka sasa ni jambo ambalo limekuwa halitolewi ufafanuzi na viongozi hao.

Aidha wamesema kuwa wanaiomba serikali ya ngazi ya juu kuweza kuingilia kati suala hilo ili kuweza kukabiliana na changamoto za kuepukana na magonjwa ya mlipuko hali ambayo inawapa hofu baadhi ya wananchi kijijini hapo kwani hawapendezwi na hali inayo zunguka maeneo hayo.


Hata hivyo wananchi hao wameongeza kuwa mbali na ukosefu wa vyoo katika maeneo ya kufanyia biashara serikali inatakiwa itambue umuhimu wa uwepo kwa bwana Afya kijijini hapo kwani changamoto hizo zinatokana na kukosa bwana afya ambae angeweza kusimamia hali ya usafi kijijini hapo nakutoa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa mazingira



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: