KIJIJI CHA MNDINDILUDEWA WALIA NA DIWANI WAO
Wananchi wa kijiji cha Mundindi katika kata ya Mundindi wilayani Ludewa hapa mkoani Njombe wamemlalamikia mganga mkuu ambaye inasemekana alikwenda hospital kujitazamia kwa kuondoka na pesa za wananchi hao za mfuko wa CHF na hakuna taarifa zozote za pesa hizo.
Wananchi hao wameyasema hayo hivi karibuni walipokuwa wakizungumza na baadhi ya waandishi wa habari katika kijiji hicho ambapo wamesema kuwa kitendo cha mganga huyo kutoka na pesa za wananchi kwao ni kero kubwa huku wakisema kuna huduma za kimsingi nyingi wananchi hao wanakosa kutokana na tukio la mganga huyo kuzulumu pesa za wananchi.
Waandishi wa habari walimtafuta mmoja kati ya waganga ambao wapo katika zahanati hiyo ili wazungumzie hilo japo kwa kifupi mmoja kati ya waganga hao alisema kuwa ni mgeni na hajui lolote kuhusu mganga huyo kutoka na pesa za wananchi za mfuko wa chf.
Wananch hao wameongeza kuwa zahanati ya kijiji hicho bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosekana kwa madawa kwa muda mrefu sana huku wakisema kuwa wanamuomba Diwani wa kata ya Mundindi mh,Wise Mgina ajitahidi kuitatua changamoto hiyo mapema ili kuwanusuru wananchi wake waliompa ridhaa ya yeye kuwa diwani.
Hata hivyo redio best fm ilimtafuta Diwani wa kata ya Mundindi ili aweze kuzungumzia changamoto ya kukosekana kwa madawa katika kituo hicho cha afya na kunabaisha kuwa yuko mbioni kufuatilia changamoto hiyo
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment