Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Idodi mkoani Iringa amefariki dunia baada ya kupigwa na radi wakati akicheza mpira uwanjani na wanafunzi wenzake.
Radi hiyo pia imejeruhi wanafunzi wengine saba na mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Idodi aliyekuwa anaokota kuni jirani na uwanja huo kabla mvua iliyoambatana na radi haijaanza kunyesha.
Tukio hilo la Ijumaa ni la pili kwa kipindi cha siku mbili ambapo siku moja kabla, mkazi wa kijiji cha Kibena Iringa vijijini akiwa anarejeha Ng’ombe kutoka malishoni aliuawa kwa radi pamoja na Ng’ombe 22 wenye thamani ya Shilingi milioni 44.
Eneo la Ndiuka Manispaa ya Iringa,waombolezaji wakiwa katika majonzi makubwa. Marehemu aliyekuwa na miaka 18 alikuwa anasubiria kumalizia mitahani yake ya kidato cha nne kwa kufanya somo moja Jumatatu ya Tarehe 16 na tayari alishawapigia simu wazazi wake wamtumie nauli ili arejee nyumb ani Jumanne baada ya mtihani wa Jumatatu.
Miongoni mwa majirani na waombolezaji wengine waliokusanyika hapa nyumbani kwa wazazi wa marehemu ni pamoja na Mkuu wa Shule ya sekondari ya Idodi, Mwl. Christopher Mwasomole na anaelezea tukio hilo lilivyotokea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Polisi Ramadhani Mungi ameto wito kwa wataalam wa vifaa vya kuzuia radi kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wananchi ili kuepusha vifo zaidi.
Wiki mbili zilizopita, upepo mkali ulioambatana na mvua, ulisababisha madhara katika vijiji viwili vilivyopo Pawaga na Idodi kwa kuezua mapaa ya nyumba kadhaa na nyumba zingine kubomolewa kabisa na kuacha familia katika nyumba hizo bila makazi
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment