Uhaba wa mashuka katika vituo vya afya mkoani Tanga umesababisha baadhi ya wagonjwa kutumia mashuka yao binafsi jambo ambalo halikubaliki kiafya.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza amekiri kuwepo kwa tatizo hilo ambalo limekuwa likisababisha usumbufu kwa wagonjwa wanaohudumiwa katika vituo hivyo.
Mahiza amesema hayo wakati akipokea msaada wa mashuka kutoka Mfuko wa Bima ya Afya NHIF kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo katika mkoa wa Tanga.
Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga inajumla ya zahanati 27 na viyuo vya afya vitatu,lakini changamoto iliyopo ni upungufu wa mashuka katika vituo hivyo kwa asilimia 20.
Mfuko wa Bima ya Afya NHIF unaona ni vyema kusaidia kutatua tatizo hili kwa kutoa mashuka kwenye baadhi ya vituo lengo likiwa ni kuiepusha jamii na adha hiyo.
Serikali inakiri kuwepo kwa upungufu mkubwa wa mashuka kwenye vituo vya afya na wakati mwingine wagonjwa ulazimika kutumia kanga na vitu vingine kujisitiri wakati wakiendelea na matibabu.
Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza kukabidhiwa msaada huo na yeye anaukabidhi kwa uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mkinga ,lakini akitaka jamii kujiunga na mfuko huo kujirahisishia huduma za matibabu.
Baadhi ya maeneo ambayo tayari mfuko huo umeshatoa msaada wa mashuka kwa ajili ya kuwasitiri wagonwa ni Tanga,Muheza pamoja na Korogwe.
0 comments:
Post a Comment