Rais Kikwete ametoa kauli hiyo wakati akifungua kiwanda cha
kuchakata gesi cha madimba kilichopo wilaya ya Mtwara vijijini mkoani
Mtwara huku akionyesha wazi hali ya umeme nchini hairidhishi.
Akiwa katika eneo hilo la kiwanda Rais Jakaya Kikwete akatumia
fursa hiyo kuitaka TPDC kutoa maji kwa wananchi wa kata ya madimba ambao
wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji na kulazimika kutumia maji ya
mabondeni ambayo si safi na salama.
Kwa upande wake waziri wa nishati na madini Mh.George Simba Chawene
amesema umeme wa gesi ni mkombozi na mara utakapokamilika utaondoa
tatizo hilo.
Amefungua kiwanda cha kuzalisha saruji cha Dangote, kiwanda cha
kuzalisha acidi cha sovo chem,sambamba na kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa shirika la nyumba la taifa na jengo la mfuko wa pensheni kwa
watumishi wa umma.
\
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment