kikosi cha timu ya milo |
Mashindano ya David Cup yamemalizika katika kata ya milo ambapo jumlya ya timu nne zilishiriki katika ligi hiyo iliyofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Milo kata ya milo wilayani Ludewa.
Mgeni rasmi katika fainali za Ligi ya David cup alikuwa ni Barnabas njenjema mtangazaji na mtayarishaji wa Vipindi mbalimbali kutoka Radio Best fm ya Ludewa.
Ambapo amewaomba wana milo na wana Ludewa kwa ujumla kuendelea kudumisha michezo ndani na nje ya wilaya ya Ludewa ili kufikia malengo ya maendeleo ndani ya wilaya ya Ludewa.
Halikadhalika ameongeza kuwa ili michezo izidi kusonga mbele katika wilaya yetu ya Ludewa ni vyema kila mmoja mpenda maendeleo ya wilaya ya Ludewa aige mfano mzuri wa Ndugu DAVID MARTIN MWINUKA mdau wa maendeleo ya Wilaya ya Ludewa katika jitiada zake za kuondoa vijana katika mazingira tatanishi wawapo mitaani.
Best fm radio kwa kushirikiana na muandaaji wa michuona ya David Cup tutakuwa pamoja katika kuhakikisha michezo inasonga mbele zaidi .
katika fainali hiyo iliyowakutanisha Mabingwa milo waliochuana na mlanje milo waliibuka kidede kwa jumla ya magoli mawili kwa moja magoli ya Milo yamefungwa na Emmenuel Mwenda,pamoja na Jamson Mhagama huku goli la mlanje likifungwa na samara..
mchezo wa nusu fainali uliwakuatanisha mavala na lipangali na Mavala kuibuka na ushindi wa magoli 2 kwa bil
Mashindano ya ligi ya Mpira ya "David Cup" yameanzishwa Rasimi mwaka huu 2015, kwa kuhusisha Timu Nne , Milo, Mavala, Lipangala na Ludende. Mashindano haya niendelevu na yameanzishwa kwa malengo yafuatayo:
1. Kufufua Mchezo wa soccer ambao umeonakana kudorora wilaya ya Ludewa nzima.
2.Kupitia Michezo hii tunamalengo ya Kupata vipaji kwajili ya kuunda Club ya Wilaya ya Ludewa,
kwa miaka ijayo, Mashindano haya yanategemea Mwitikio wa Team nyingi zaidi kushiriki.
Tutafurahi kuona Timu nyingi zinajitokeza kushiriki mashindano haya na Tutayaboresha zaidi
Tutaboresha zawadi ya mshindi wa Kwanza na washiriki kwa ujumla, Tutatoa Jeasy, Mipira na Usafiri
wakati wa Mashindano.
3. Lengo lingine la michezo hii ni kuwaweka vijana pamoja , tukiwa tunakutana katika michezo tujifunze kuzungumza na kubadilisha fulsa za Kimaendeleo. Vijana wakijiunga na Timu za mipira wataondokana na
mambo yasiyo ya msingi kwenye jamii,
4. Michezo hii inalengo la kuwaondoa Vijana kujiingiza kwenye magenge, Mfano: ya Kushiriki Ngono zembe, wizi, na Ulevi , Tunapenda vijana baada ya kazi washiriki sana kwenye michezo inayojenga afya zaidi.
Napenda kuwapongeza Washiriki wote walijitokeza kushiri na Sisi katika Mashindano haya.
Mashindano haya ni ya wana Ludewa wote hayahusiani na mambo ya kisiasa,Kabila wala udini nawakaribisha vijiji vyote kuungana nasi katika malengo niliyo yazungumza hapo Juu.
Nachukua nafasi hii Kuwapongeza Team zilizofanya Vizuri na Zawadi zinatolewa kama ifuatavyo
i) Mshindi wa Kwanza Tshs 400,000/= na Mpira
ii)Mshindi wa Pili Tshs 200,000/= na mpira
iii) Mishindi wa Tatu 100,000/= na Mpira
iv) Mshiriki wa nne anajipatia Mpira,
Mipira hii ilishatolewa kabla ya kuanza mashindano
Katika kundeleza Michezo ni Mimi ndugu yenu
DAVID MARTIN MWINUKA
Blogger Comment
Facebook Comment