Mgombea aliyetabiriwa kifo kumbe ni Mtikila
MTABIRI
maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein, amesema utabiri wake
alioutoa mwaka 2014 kwamba mgombea urais mmoja atafariki dunia ghafla
kabla ya uchaguzi, umetimia baada ya kifo cha Mchungaji Christopher
Mtikila na kuwaacha salama wagombea Edward Lowassa na Dk. John Magufuli.
Maalim
Hassan aliyasema hayo alipozungumza na gazeti la Uwazi juzi ambapo
alisisitiza kuwa utabiri wake alioutoa Desemba 28, 2014 katika mkutano
wake na waandishi wa habari ofisini kwake, haukumlenga mtu.
Mchungaji
Mtikila ambaye alikuwa akigombea urais kupitia Democratic Party (DP)
kabla ya kuenguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), alifariki dunia
Oktoba 4, 2015 kwa ajali ya gari kijijini Msolwa, Chalinze, mkoani Pwani
akitokea Njombe.
“Nilipoutoa
utabiri ule mengi yalisema na watu wakawataja wagombea fulani, lakini
niliwaambia kwamba utabiri haulengi mtu na sasa umempata Mchungaji
Mtikila.
“Mtikila
alikuwa mgombea urais, alichukua fomu na watu wakaona akiwa na mkoba
kama wa wagombea wenzake, akakataliwa na tume lakini akakata rufaa…
angeweza pia kushinda rufaa yake,” alisema Maalim Hassan.
Aliongeza
kuwa, mara baada ya utabiri wake alipigiwa simu na makada wa vyama
viwili – Chama cha Mapinduzi (CCM) waliodai kuwa mgombea wao Dk.
Magufuli haumhusu na wale wa Chadema nao wakasema mgombea wao, Lowassa
hawezi kuchuliwa hivyo – akawajibu wote kwamba utabiri wake haumlengi
mtu.
“Niwahakikishie
wananchi kwamba, kinyota wagombea wote wa urais waliobaki sasa wako
salama na watashiriki kuchagua viongozi Oktoba 25, mwaka huu,” alisema
Maalim Hassan
Mgombea aliyetabiriwa kifo kumbe ni Mtikila By Edwin Moshi at Tuesday, October 13, 2015 MTABIRI maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein, amesema utabiri wake alioutoa mwaka 2014 kwamba mgombea urais mmoja atafariki dunia ghafla kabla ya uchaguzi, umetimia baada ya kifo cha Mchungaji Christopher Mtikila na kuwaacha salama wagombea Edward Lowassa na Dk. John Magufuli. Maalim Hassan aliyasema hayo alipozungumza na gazeti la Uwazi juzi ambapo alisisitiza kuwa utabiri wake alioutoa Desemba 28, 2014 katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake, haukumlenga mtu. Mchungaji Mtikila ambaye alikuwa akigombea urais kupitia Democratic Party (DP) kabla ya kuenguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), alifariki dunia Oktoba 4, 2015 kwa ajali ya gari kijijini Msolwa, Chalinze, mkoani Pwani akitokea Njombe. “Nilipoutoa utabiri ule mengi yalisema na watu wakawataja wagombea fulani, lakini niliwaambia kwamba utabiri haulengi mtu na sasa umempata Mchungaji Mtikila. “Mtikila alikuwa mgombea urais, alichukua fomu na watu wakaona akiwa na mkoba kama wa wagombea wenzake, akakataliwa na tume lakini akakata rufaa… angeweza pia kushinda rufaa yake,” alisema Maalim Hassan. Aliongeza kuwa, mara baada ya utabiri wake alipigiwa simu na makada wa vyama viwili – Chama cha Mapinduzi (CCM) waliodai kuwa mgombea wao Dk. Magufuli haumhusu na wale wa Chadema nao wakasema mgombea wao, Lowassa hawezi kuchuliwa hivyo – akawajibu wote kwamba utabiri wake haumlengi mtu. “Niwahakikishie wananchi kwamba, kinyota wagombea wote wa urais waliobaki sasa wako salama na watashiriki kuchagua viongozi Oktoba 25, mwaka huu,” alisema Maalim Hassan
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko