Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekosoa
kimya cha serikali za Magharibi na taasisi zinazodai kutetea haki za
binadamu kuhusu maafa ya machungu ya Mina. Ayatullahil Udhma Ali
Khamenei amesema maafa ya kusikitisha sana na ya kutisha ya Mina ni moja
kati ya mitihani ya Mwenyezi Mungu na kusisitiza kuwa, msiba huo mkubwa
haupaswi kusahauliwa. Amesema kuwa chombo cha udiplomasia na Jumuiya ya
Kusimamia Hija vina jukumu la kufuatilia kadhia hii ipasavyo. Kiongozi
Muadhamu wa Mapinduzi ambaye alikuwa akihutubia hadhara ya wafanyakazi
na wasimamizi wa msafara wa ibada ya Hija ameashiria majukumu ya
serikali mwenyeji mkabala na kupoteza maisha Waislamu elfu saba na
kubainisha kuwa, baada ya kujiri tukio hilo, ulimwengu wa Kiislamu
ulipasa kupaza sauti moja na kulalamikia jambo hilo, hata hivyo
inasikitisha kamba hakuna sauti iliyosikika ghairi ya sauti ya Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran na kwamba hata serikali ambazo mahujaji wao ni
miongoni mwa watu walioaga dunia huko Mina, hazikuwasilisha malalamiko
inavyotakikana kuhusiana na maafa hayo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema,
kufuatilia maafa ya Mina na kufanya mazungumzo na serikali za nchi
mbalimbali ili kubainisha umuhimu wa kilichotokea na kuchunguza njia za
kuzuia kutokea tena maafa kama hayo ni jukumu muhimu la maafisa husika,
hususan chombo cha udiplomasia cha Iran. Ayatullah Khamenei ameongeza
kuwa, ni wazi kwamba maafa ya Mina yametokana na upuuzaji wa serikali
mwenyeji, lakini kwa hali yoyote ile, suala hili si suala la kisiasa,
bali ni kadhia inayowahusu maelfu ya Waislamu ambao wameaga dunia wakati
wakiteleza ibada na amali ya Hija huku wakiwa katika vazi la Ihram na
kwamba na suala hili ni linapasa kufuatiliwa kwa jadi.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment