MGOMBEA
wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli pamoja
na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), pamoja na vyama vinaunda Ukawa, Edward Lowassa leo
wameshindwa kuhudhuria mdahalo maalumu wa wagombea urais ulioandaliwa na
Mkikimkiki kutokana na sababu mbalimbali. Mdahalo
huo ulikuwa unajadili mambo mbalimbali kama vile uchumi,katiba ya
uchaguzi, malengo endelevu ya umoja wa mataifa, katiba inayopendekezwa,
viashiria vya uvunjifu wa amani nchini, uchumi na huduma za kijamii
kwenye sekta ya afya.
Wakizungumza
kwenye mdaharo huo Dar es Salaam wagombea nafasi za urais kupitia vyama
vya ACT-wazalendo, ADC na TLP walikuwa na mengi ya kuelezea kuhusu
mstakari wa taifa la Tanzania. Mgombea
urais wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chief Lutasola
Yemba akijibu swali lilioulizwa kwamba wagombea hao watawezaje kuondoa
rushwa kwa wanafunzi pindi wanapotafta ajira endepo akipata ridhaa ya
kuingia madarakani alisema.
SWALI
Mtawezaje kuondoa tatizo la rushwa kwa wanafunzi waliokoswa nafasi za
kazi kwa maadai ya kukoswa uzoefu huku wakiombwa chochote kabla ya
kupewa ajira rasmi.
Chief
Yemba alisema Serikali ya ADC itahakikisha wanafunzi wanatakiwa kupata
kazi punde baada ya kuhitimu masomo yao bila kusubiri kupata uzoefu huku
akiwa anafanya kazi katika taaluma yake hata kama ni kwalipo kidogo na
kwa baadae atakuwa na uzoefu mkubwa.
Kwa
upande wake mgombea urais kupitia Chama cha ACT- wazalendo ,Anna
mghira akijibu swari hilo alisema rushwa ni utamaduni lakini chama cha
ACT- wazalendo kiatatoa elimu ya rushwa tangu wakiwa wadogo,ambapo
itakuwa ni utamaduni wa mwanafunzi tangu akiwa mdogo.
”Pia
tumeweka mikakati ya utekelezaji ambapo ni namna tutakavyoshughulika na
mikakati mbalimbali huku tukiwajumlisha wananchi kutoa maoni yao na
kurudi kwetu kiutekelezaji ili kuziba mianya ya rushwa ,”alisema
Mgombea
urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Nghwira
(kulia), na Mgombea nafasi hiyo kupitia Chama cha Alliance for
Democratic Change (ADC), Chifu Litayosa Yemba wakijibu maswali
mbalimbali katika mdahalo wa wagombea urais ulioandaliwa na Taasisi ya
Twaweza Dar es Salaam leo. Hata hivyo wagembea nafasi hiyo kupitia Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Dk.John Magufuli na Edward Lowassa kupitia Chadema
hawakuweza kuhudhuria kwa sababu mbalimbali.
Waongozaji wa mdahalo huo wakiwa kazini.
Wadau wakiwa kwenye mdahalo huo.
Raia wa kigeni na wadau wengine wakifuatilia mdahalo huo.
Mdahalo ukiendelea.
Vijana wakiwa kwenye mdahalo huo.
Na Dotto Mwaibale
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment