LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE NYUMBANI EUROPA LEAGUE, SPURS WAPIGWA



LIVERPOOL imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Rubin Kazan katika mchezo wa Kundi B michuano ya Europa League usiku huu.
Na ilibidi timu ya kocha Mjeruman, Jurgen Klopp itoke nyuma kupata sare hiyo baada ya Emre Can kusawazisha dakika ya 37, kufuatia Marko Devic kuanza kuwafungia wageni dakika ya 15 Uwanja wa Anfield.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, FC Sion imeshinda ugenini 1-0 dhidi ya Bordeaux, bao pekee la Leo Lacroix dakika ya 21 Uwanja wa Matmut Atlantique.
Emre Can akiifungia Liverpool bao la kusawazisha Uwanja wa Anfield PICHA ZAIDI GONGA HAPA

Molde imeshinda 3-1 dhidi ya Celtic mchezo wa A, mabao yake yakifungwa na Ola Kamara dakika ya 11, Vegard Forren dakika ya 18 na Mohammed Elyounoussi dakika ya 56, huku bao la wageni likifungwa na Kristian Commons dakika ya 55.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Fenerbahce imeshinda 1-0 dhidi ya Ajax, bao pekee la Jose Fernando Viana de Santana dakika ya 89 Uwanja wa Sukru Saracoglu.
Villarreal imeshinda 4-0 dhidi ya Dinamo Minsk katika mchezo wa Kundi E, mabao ya Cedric Bakambu dakika ya 17 na 32, Roberto Soldado dakika ya 61 na Eric Bailly dakika ya 70 Uwanja wa 
El Madrigal.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, SK Rapid Wien imeshinda 3-2 dhidi ya Viktoria Plzen, mabao yake yakifungwa na Steffen Hofmann dakika ya 34, Louis Schaub dakika ya 52 na Thanos Petsos dakika ya 67, wakati mabao ya wapinzani wao yamefungwa na Michal Duris dakika ya 12 na Patrik Hrosovsky dakika ya 76.
Napoli imeshinda 4-1 ugenini dhidi ya FC Midtjylland mchezo wa Kundi D mabao yake yakifungwa na Jose Callejon dakika ya 19, Manolo Gabbiadini dakika ya 31 na 40 na Gonzalo Higuain dakika ya 90 na ushei. Bao pekee la Midtjylland limefungwa na Martin Pusic dakika ya 43.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Legia Warsaw imelazimishwa sare ya 1-1 Club Brugge tena wakichomoa kupitia kwa Michal Kucharczyk dakika ya 51, baada ya Davy de Fauw kuanza kuwafungia wageni dakika ya 39.
Slovan Liberec nayo imelazimishwa sare ya 1-1 na FC Groningen katika mchezo wa Kundi F, bao lao likifungwa na Kevin Luckassen dakika ya 87 na wageni wakisawazisha kupitia kwa Danny Hoesen dakika ya 96.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Sporting Braga imeshinda 3-2 dhidi ya Marseille mabao yake yakifungwa na Ahmed Hassan dakika ya 61, Wilson Bruno Naval Costa Eduardo dakika ya 77 na 
Alan Osorio Costa Silva dakika ya 88, wakati ya wageni yamefungwa na Romain Alessandrini dakika ya 84 na Michy Batshuayi dakika ya 87.
Katika Kundi C, Borussia Dortmund imeshinda 3-1 ugenini dhidi ya FK Qabala, mabao yake yote yakifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 31, 38 na 72, huku bao pekee la wenyeji likifungwa na Luiz Paulo Hilario dakika ya 93. Mchezo mwingine wa kundi hilo, PAOK Salonika imelazimishwa sare ya 0-0 na FK Krasnodar.
Monaco imeshinda 1-0 dhidi ya FK Qarabag katika mchezo wa Kundi J, bao pekee la Lacina Traore dakika ya 70, wakati RSC Anderlecht imeifunga 2-1 Tottenham Hotspur katuika mchezo mwingine wa kundi hilo, mabao yake yakifungwa na Guillaume Gillet dakika ya 13 Stefano Okaka dakika ya 75, huku bao pekee la Spurs likifungwa na Christian Eriksen dakika ya nne.
Sporting Lisbon imeifumua 5-1 Skenderbeu Korce katika mchezo wa kundi H, mabao yake yakifungwa na Alberto Aquilani kwa penalti dakika ya 38, Fredy Montero kwa penalti pia dakika ya 41, Matheus Pereira dakika ya 64 na 77 na Tobias Pereira Figueiredo dakika ya 69, huku bao la kufutia machozi la wageni likifungwa na Bajram Jashanica dakika ya 89.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Lokomotiv Moscow imelazimishwa sare ya 1-1 na Besiktas, wakitangulia kufunga kupitia kwa Maicon Marques Bitencourt dakika ya 54, kabla ya Mario Gomez kusawazisha dakika ya 64.
Lazio imeshinda 3-1 dhidi ya Rosenborg katika mchezo wa Kundi G, mabao yake yakifungwa na Alessandro Matri dakika ya 28, Felipe Anderson Pereira Gomes dakika ya 54 na Antonio Candreva dakika ya 79, huku bao pekee la wageni likifungwa na Alexander Soderlund dakika ya 69.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, St Etienne imeshinda 1-0 ugenini dhidi ya Dnipro Dnipropetrovsk, bao pekee la Romain Hamouma dakika ya 44. 

Anderlecht's Olivier Deschacht screams in pain as Lamela slides in from behind to make a challenge which is penalised by the referee
Olivier Deschacht wa Anderlecht akiugulia maumivu baada ya kukwatuliwa na Lamela kwa nyuma na kusababisha penalti PICHA ZAIDI GONGA HAPA
FC Schalke 04 imelazimishwa sare ya 2-2 na Sparta Prague katika mchezo wa Kundi K mabao yake yakifungwa na Franco Di Santo dakika ya sita na 
Leroy Sane dakika ya 73, wakati ya wageni yamefungwa na Kehinde Fatai dakika ya 50 na David Lafata dakika ya 63.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, APOEL Nicosia imeshinda 2-1 dhidi ya Asteras Tripolis mabao yake yakifungwa na Fernando Cavenaghi kwa penalti dakika ya 43 na Carlos Roberto da Cruz Junior dakika ya 59, huku bao pekee la wageni likifungwa na Brian Lluy dakika ya nane.
Partizan Belgrade imefungwa 2-0 nyumbani na Athletic Club katika mchezo wa Kundi L, mabao ya Raul Garcia Escudero dakika ya 32 na Benat Etxebarria Urkiaga dakika ya 85.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, AZ nao imefungwa 1-0 nyumbani na FC Augsburg bao pekee la Piotr Trochowski dakika ya 43.
Fiorentina nayo imefungwa 2-1 nyumbani na Lech Poznan katika mchezo wa Kundi I, bao lao likifungwa na Giuseppe Rossi dakika ya 90 baaada ya wageni kutangulia kwa mabao ya Dawid Kownacki dakika ya 65 na Maciej Gajos dakika ya 82.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, FC Basel imefungwa 2-1 nyumbani na Belenenses bao lake likifungwa na Michael Lang dakika ya 15, kabla ya wageni kunufaika na mabao ya Luis Leal dakika ya 27 na Jailton Alves Miranda dakika ya 46.



Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: