Hatimaye,
Halmashauri ya manispaa ya Ilala imekifunga rasmi kiwanda bubu
kinachosindika sehemu nyeti za Ng'ombe Dume, kutokana na kufanya kazi
zao katika makazi ya watu,huku kukiwa na mazingira machafu na
kusababisha harufu kali katika eneo la Tabata bima mtaa wa umoja jijini
Dsm.
Kufungwa
kwa kiwanda hicho Bubu ambacho pia kimekuwa kikikusanya pembe za
ng'ombe na kusafirisha nchini China, kumetokana na malalamiko kutoka
wananchi ambao walikuwa wakilalamikia harufu kali, inzi na mazingira
machafu ya eneo hilo.
Aidha
wamiliki hao raia wa kichina pamoja na kufungiwa rasmi wamepigwa faini
ya shilingi millioni kumi, kutokana na kuendesha shughuli zao katika
mazingira machafu hali inayoweza kueneza magonjwa.
Mmoja
wa wafanyakazi katika eneo hilo amesema nyeti hizo za ng'ombe zimekuwa
zikiletwa na kukaushwa eneo hilo na baadae kusafirishwa kwenda china kwa
ajili ya kutengeneza dawa za kuongeza nguvu za kiume maarufu Viagra.
Katika
eneo hilo pia kimebainika kiwanda cha kutengeneza vitu mbali mbali vya
ndani ikiwemo sahani za plastic huku zikiwa zimebandikwa lebo kutoka
china ambapo baada ya kutakiwa kuonyesha vibali walishindwa kuonyesha
na kudai kiwanda hicho kipo katika hatua za majaribio
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko