RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu
wake, Dk. Mohammed Gharib Bilal na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Hamad wamejitokeza leo kwenye
viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kutoa heshima zao mwisho
kwenye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Democratic Party, Mchungaji
Christopher Mtikila.
Marehemu
Mtikila alikuwa mwanasiasa mkongwe aliyefariki dunia kwa ajali ya gari
Oktoba 4 mwaka huu katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze Mkoa wa Pwani,
wakati akirejea Dar es Salaam kutokea Njombe alikokuwa amekwenda kufanya
mkutano wa kampeni.
Viongozi
wa vyama vya siasa, taasisi na mashirika mbalimbali yalipata fursa ya
kutoa shukurani zao za pekee kuzungumzia historia ya marehemu enzi za
uhai wake ambapo kila mmoja alimzungumzia Mchungaji Mtikila alivyokuwa
kiongozi shujaa, mwenye maamuzi na kusimamia kile alichokuwa akikiamini.
Akitoa
salamu za rambirambi Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Jaji, Francis
Mutungi amesema kuwa marehemu ameacha pengo kubwa kwa chama cha DP,
kwani alikuwa kiongozi aliyekuwa akisimamia haki na kile alichokuwa
akiamini na alikuwa hapindishwi na mtu yeyote na alikuwa ni mmoja wa
wanaharakati wa haki za binadamu.
Alisema
kuwa Mtikila alikuwa mwanaharakati asiyependa maandamano mwenye
kuchukua maamuzi ya kwenda mahakamani kwa ajili ya kupata haki
anayoitaka na ndiye alikuiwa mwanzilishi wa kudai mfumo wa vyama vingi
mwaka 1992.
Mwili
wa marehemu umesafilishwa kwenda Ludewa, Njombe ambapo wakazi wa mkoa
huo watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kuzikwa.
Anatarajiwa kuzikwa kesho.
Mwili ukiwa katika jeneza tayari kwa kuagwa.
Rai wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete akisaini katika kitabu cha maombolezo.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akisaini kwenye kitabu cha maombolezo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari, Maalim Seif Hamad Sharif akisaini kitabu cha maombolezo.
Rais Kikwete (katikati) akiwa kwenye msiba huo kabla ya kuuaga mwili wa Mch.Christopher Mtikila sambamba na viongozi wengine.
Dk.Bilal akiwapa pole wafiwa.
Jaji Francis Mutungi akitoa salamu za pole kwa wafiwa.
Dk.Bilal akitoa heshima zake za mwisho.
Gari lililobeba mwili wa marehemu Mch.Christopher Mtikila likiwasili viwanja vya Karimjee, Dar.
Geojina Mtikila, mke wa marehemu akisaidiwa mara baada ya kushuka katika gari lililokuwa limebeba jeneza lenye mwili wa mumewe.
Sehemu ya wanandugu walipokuwa wamekaa wakati wa kuuaga mwili wa Mtikila.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment